Karma is real. Kisa cha Binti na "Mtu Asiyejulikana"

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,860
Kisa hiki ni cha kweli kabisa na kimetokea hapa Tanzania.

Mtu Asiyejulikana alimuoa binti ya watu, akakaa nae kwa miezi michache sana, akamucha kwa kejeli akaenda kuoa binti mwingine. Huyu aliyeachwa akaanza kuugua maradhi ya kisukari, akaumwa sana, figo zikafeli, Sasa anaishi kwa matibabu ya kusafisha damu kila wiki. Mtu Asiyejulikana akapewa assignment aende kanda ya ziwa kumshughulikia na kumpoteza mfanyabiashara mkubwa wa mabasi.

Bahati mbaya mfanyabiashara akawa vizuri kuliko wao, akawamiminia risasi za kutosha. Mtu asiyejulikana akaathirika uti wa mgongo, mpaka Sasa yuko South Africa kitandani.

Malipo kwa yale tunayowatendea wenzetu tunayapata hapa hapa duniani. Tangu binti augue Mtu Asiyejulikana hakuwahi kwenda kumsabahi wala kumjulia hali. Hujafa hujaumbika.

UPDATES:-
Mtu Asiyejulikana karudishwa nchini, atalala kitandani maisha yake yote. Idara wa Watu wasiojulikana wameshamwandikia barua ya kumfuta kazi, lakini kijana amegoma kuisaini.
 
Huyu shushushu anayeongelewa namjua, namjua vizuri Sana na kisa cha kumuacha dada wa watu hadi akaumwa nusu ya kufa, na yeye Sasa yamemkuta, yuko kitandani. Tujifunze kutenda wema
Daah toka kipindi hicho bado yupo hospital??!!
 
Back
Top Bottom