Asante sana Bi. Rose na Bw. Alnashir kwa mawaliko wenu. Nimefurahi sana kukuta post yenu katika Jamii Forum. Kama mtakumbuka, nilishawahi kufika katika hoteli yenu na nililala hapo siku mbili. Katika holidays zangu zote, sehemu niliyokaa na kujihisi niko nyumbani ni katika hoteli yenu kwani mlinikarimu vizuri sana. Bado nawashukuru sana kwa msaada wenu mkubwa mlionipa katika kuandaa spice tour na dolphin safari. Hoteli yenu pia ni safi sana na vyumba vyake vina hadhi ya juu mno. Bei zenu pia ni nafuu sana kilinganisha na hoteli zipatikanazo Stone town. Lazima nikiri kwamba milo ya asubuhi (Breakfast) niliyopata hapo kwenu ulikuwa ni mzito na yenye ubora. Pia, wafanyakazi wenu ni wakarim, wacheshi na wamebobea katika kazi yao. Sitosita kuwashawishi ndugu, jamaa na marafiki kufikia hapo kwenu mara watakapo kitembelea kisiwa cha Unguja hapo Zanzibar-Stone town. Ni mimi, Steve Robert (Kutoka Dar-es-salaam).