Karibuni tena majimboni Wabunge

Zinjathropus

Member
Oct 14, 2018
13
2
*KARIBUNI TENA MAJIMBONI WAH. WABUNGE*

Kwa mujibu wa katiba yetu ya JMT '77 kazi/wajibu/jukumu la Mbunge ni:

1:Ni kiungo/daraja kati ya *wananchi na serikali*

Maana yake anao wajibu wa kuhakikisha anawaunganisha wananchi na serikali yao kwa *kuyachukua matatizo/changamoto za wananchi wanazokutana nazo katika mazingira yao ya kimaisha na kuzipeleka serikalini* kupitia bunge ili serikali iweze kwenda kwa wananchi na kutatua matatizo yao ambayo eidha serikali yenyewe iliahidi au kuibuliwa na wananchi wenyewe.

Pia Mbunge ni wajibu wake *kushirikiana na wananchi* katika kutafuta njia na vyanzo/nyenzo zitakazosaidia kutatua changamoto muhimu kwa wananchi.

Mbunge anapaswa kuwa *sauti ya wananchi* kwa serikali, ndio maana alichaguliwa ili akawawakilishe kwa serikali kupitia bunge.

2:Mbunge ni *mshauri na msimamizi* wa serikali kwa niaba ya wananchi

Yaani Mbunge anapaswa kuhakikisha *kodi ya mwananchi inayokusanywa na serikali* inarudi kwa wananchi ili ikatekeleze mahitaji ya wananchi, kwa maana nyingine Mbunge ni msimamizi wa kodi ya wananchi.

Ukiwa Mbunge, unapaswa kutambua kuwa huo ubunge sio wako, ni wa wananchi !!

Wao ndio *waliokuajiri* ili ukawatumikie wao na wao ndio wanaokulipa mshahara wako kupitia kodi zao.

Ubunge wako ni *mkataba uliokubali kuutekeleza kwa kipindi cha miaka mitano (05)* kwa kuwawakilisha waajiri wako (wananchi)

*Karibuni tena majimboni*

Ni miaka minne sasa tangu sie wananchi tulipowatuma mkatutumikie bungeni, umebaki mwaka mmoja kwenu wa kututumikia kabla ya *kurudi tena kwetu ili tukae mezani na "kuurinwuu" mkataba wetu.

Tutakuja kuambizana na kupima namna mlivyoutekeleza mkataba wetu kwa kuupima utumishi wenu kwetu.

*Wengi wenu mmejisahau*

Kwa miaka mingi nyie Wah. sana Wabunge wengi wenu mmekuwa mkitulaghai sana sie waajiri wenu kwa muda mtefu, pengine mmekuwa mkitumia miaka yenu minne kutulaghai, kisha mwaka wa mwisho mnarudi kutafuta huruma kwetu kwa kuwa mnajua wengi wetu hatuna uelewa, mnajua mkirudi kwa njia za "danganya toto" tunadanganyika

Miaka minne *hujawahi kurudi kwetu* kutusikiliza tukupe kero zetu ukazipeleke serikalini zitatuliwe

Miaka minne umeitumia kuchuma kupitia *ajira tuliyokupa* bila kujali kuwa kuna tuliokupa hiyo ajira.

Miaka minne umeitumia *kugonga meza* kwa kila unacholetewa na serikali bila *kujishughulisha kukisoma ili utambue umuhimu wake wa waajiri wako na uweze kuhoji juu ya maslahi ya mwananchi wako kwa kile ulicholetewa na serikali*

Miaka minne umeitumia kwa *kuungana na serikali katika kutunga na kupitisha sheria kandamizi na nyonyaji kwa mwananchi wako !!* badala ya kuhoji umuhimu wa sheria hizo kwa mwajiri wako aliyekutuma ukamtetee.

Miaka minne umeitumia *kutengeneza matatizo* kwenye maeneo yetu kwa kutokuyashughulikia ili ukirudi ukute yameongezeka zaidi na uje *uyatumie kuomba kura kwa mara nyingine* (Unatengeneza tatizo ili uje ujifanye unalitatua), kwa kuwa unajua ukija na *fulana, kofia, madebe ya pombe, chumvi n.k* tutasahau matatizo yote na tutakushangilia na kukubeba juu juu Kama shujaa wa vita !!

*Mmeanza kurudi*

Nimeona mkutano wa Mh. Sana Mbunge wa Mufindi Kaskazini, hotuba yake sijaishangaa kwa kuwa natambua fikra za Wabunge wa sampuli yake wanavyotuchukulia sie wananchi wa taifa hili, ila nimeshangaa kuona kuwa ati ni kweli hajui wajibu wake au alisahau ??

Kwa wananchi wa Miaka ya leo, hii hotuba ya Wabunge wa aina hii tunaishangaa zaidi kuliko kutowashangaa kwa wao kudhani kuwa bado sie ni wakudanganywa.

Mbunge anashangaa ni kwanini barabara mbovu hazipitiki !! Miaka minne ya kuwatumikia wananchi wake, alikuwa wapi ??

Mbunge anashangaa kwa nini serikali imetoa mill. 30 tuu za ujenzi wa barabara nyenye urefu wa km 61 !! Yeye analalamika kwa wananchi badala ya kuilalamikia na kuihoji serikali akiwa bungeni sasa analalamika kwa wananchi !! Na wananchi wakalalamikie wapi ??

Sasa anasema amekwishapata pesa mill. 800 za ujenzi wa hiyo barabara ya kata, baada ya Miaka minne !! Kwanini sasa ? Kama Miaka minne ilishindikana kujenga hata nusu kilomita, huu mwaka mmoja ndo itawezekana kujenga km 61 ?

Uhalisia ni kwamba anarudi kwa ajili ya kuanza kuyaibua matatizo aliyoyawekeleza kwenye kibubu ili aanze kuyatumia Kama njia ya kuandaa mazingira ya kuungwa mkono kwa mara nyingine, na si Kama kweli anataka kuyatatua !! Kwa kuwa anajua kuwa wananchi tutasahau kwa uelewa wetu mdogo !!

*Nafasi ya Mufindi kiuchumi*

Wilaya ya Mufindi, ni mingoni mwa wilaya tatu zinazoongoza *kuchangia pato la taifa*

Mazao makuu ya *miti, chai, viazi n.k* ni mazao yanayopatikana kwa wingi kutoka wilaya hiyo na kulilisha taifa,

Licha ya Wilaya ya Mufindi kuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa, uhalisia wa maisha ya watu wake ni Kama watu wanaoishi kwenye wilaya kame Kama kongwa n.k, ni Kama hakuna wanachokizalisha !!

Maeneo mengi ya Wilaya ya Mufindi, ni Kama kisiwa, uchumi wao mbovu kwa kuwa hakuna miundombinu inayowaunganisha na maeneo mengine muhimu ili kuweza kusafirisha mazao yao Kama viazi n.k kwenda masokoni, maeneo mengi hayaingiliki kwa kuwa hayana barabara, ni Kama kisiwa !!

Wilaya ya Mufindi, yenye majimbo matatu, licha ya majimbo yote *kuongozwa na chama kinachounda serikali* ambayo ndiyo inayokusanya mapato ya Wilaya hiyo na taifa, bado wananchi wake ni Kama hawana Wabunge waliowatuma kuwawakilisha !!

Kutembea na ilani mifukoni bado hakujawasaidia Wabunge hao kutekeleza majukumu yao vyema ya kuisimamia serikali na kuwasemea wananchi serikalini kupitia bunge kwa maslahi ya maendeleo ya wananchi wao.

*Wananchi wanalalamika*

Kwenye mkutano wa Mbunge huyo wa Mufindi Kaskazini, wananchi wanalalama juu ya maendeleo mabovu kwenye maeneo yao, nyie mnaolalamika sasa, baada ya Miaka minne, mmechelewa !!

Maana huu sio muda wa Wabunge hawa ambao ndo kwanza wanashangaa kwanini maendeleo mabovu kusema huu mwaka mmoja watawatatulieni matatizo yenu, yaani hamjashiba kwenye sinia,
mnataka kushiba kwenye kisosi ? hilo halitawezekana !!

Huu mwaka mmoja ambao wao wanautumia kuja kuibua matatizo waliyoyawekeleza ili uwe mtaji wao wa kuomba kura kwetu, Ni vema nasi yukautumia kwa *kuwahoji na kuwapima* namna walivyoitumia Miaka yao minne katika kutimiza wajibu wao katika kututatulia matatizo yetu kwa manufaa yetu.

Ni muda wa kuwaweka kikaangoni ili tupime kuwa *wanafaa tena kuendelea kuingia mkataba wa kututumikia ama lah !!*

*Ni muda wetu sisi wananchi kuwahoji juu ya utumishi wenu*

*Karibuni tena majimboni*

*Prosper Lazaro*

*@prosperlazaro94@gmail.com*
 
Watakuja karibuni kuweka mazingira ya ninyi kuwapa ridhaa ya kuwawakilisha kwa miaka mitano zaidi.
 
Back
Top Bottom