Karibuni kwenye movement #foundinTanzanianotKenya

ntita

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
513
285
Wanajamvi..

Hii ni movement mpya ambayo tumeamua kuianzisha katika mitandao ya kijamii baada ya kuudhiwa na tabia ya wakenya kutumia vivutio vyetu vya kitalii kujitangaza hii itasaidia..

1. Kutangaza vivutio vya kitalii katika taifa letu kama njia ya kushiriki ujenzi wa taifa letu badala ya kusubiri serikali ifanye kila kitu.

2. Kuwaonyesha wakenya kua tumeudhiwa na tabia yao ya uongo na uroho wa raslimali..

Ili kushiriki movementi hii jitahid kuposti kivutio hata kimoja kwa siku katika mitandao ya kijamii huku ukiweka hashtag [HASHTAG]#foundinTanzanianotKenya[/HASHTAG]..

Tunaomba mtuunge mkono kwa sisi si watu maarufu sana hivyo marafiki tunaowafollow na wanaotufollow si wa kimataifa sana ila kwa kua humu kuna watu wa kada tofauti tofauti ni imani yetu kua movement hii itafika mbali na tutafanikiwa kuitangaza nchi yetu na kuwaumbua wakenya kwa uroho wao..

Asanteni kwa kuwa naamini mtatuunga mkono.
 

Attachments

  • 1456732852225.jpg
    1456732852225.jpg
    41.4 KB · Views: 33
hakikisha unashiriki movement hii kwa ajili ya MAMA TANZANIA.
 
tumebadilisha hashtag.. sasa ni [HASHTAG]#proudtobeTanzanian[/HASHTAG]
 
tushirikiane pamoja.. [HASHTAG]#foundinTanzanianotKenya[/HASHTAG]
 
Acheni majingu fanyeni kazi Tanzania itajitangaza kwa sisi kufanya kazi, Kenya wana njia nyingi sana za kujitangza acheni ujinga fanyeni kazi jamaa zangu.

1. Kenya ni moja ya Top 5 kwa riadha duniani wachezaji wao wanabeba medali kila kukicha hiyo tu inatosha kuwatangaza dunaia nzima

2. Shirika lao la ndege lina ruka hadi Ulaya na Asia na mwezi wa tano wanaruka hadi USA sasa hapo unategema nini?

3. Kenya ni nchi ya pili kwa kuwekeza Tanzania yaani wao wamewekza zaidi Tanzania kuliko hata wazungu wana Mabenki kama KCB na Equity bank, wana mashule, wana Mahoteli, Viwanda na kadhalika je sisi tumewkeza nini kwao?

Huu muda wa kupiga majungu fanyeni kazi, tunapenda sana majungu wakati wenzetu wanapiga kazi, Kenya inajulikana sana Dunini kuliko sisi na hiyo sio bahati mbaya bali ni wao wenyewe na vitu kama Riadha inaogoza kuwatangaza nje kimataifa.
 
hakikisha unashiriki movement hii kwa ajili ya MAMA TANZANIA.
siwezi shiriki huu upuuzi,

Tanzania itajitangaza kwa sisi kufanya kazi. Hebu nikuulize unazani ni kwa nini Kenya ni ya pili kwa kuwekeza Tanzania? je hiyo movement itabadilisha ukweli?
 
Mnataka kujitangaza Twitter... Kweli nchi hii ming'ombe ni wengi sana.. Tufanye kazi tuache ngono na upuuzi...
 
Usichokoze mambo wakati hujui jambo, hawa Wakenya inasemekana zamani huko nyuma Kilimanjaro ilikua iko Kenya Je kuna makubaliano ya kugeukana hapo? Je kulikua na mikataba yoyote au walipeana kwa mdomo tuu?

Je muda wa mikataba umemaliza? Pengine sisi Watz ndio hatuna haki, hapa kwanza Serikali Itoe angalizo mambo mengine baadae.
 
Neno ngono kwenye hii mada imekujaje

Wewe ulitaka tujatangaze wapi!!
Hao wakenya wanajitangaza wapi??

Kenge wewe watu wanatumia pesa na rasilimali watu kujitangaza sio kwenda twitter kuandika ujinga mpuuzi kabisa wewe...
 
Hii nchi ming'ombe mingi sana... Wanaacha kuhoji kwanini mabalozi wetu walioko Kenya na US wasilipinge hili hadharani hao wanaaminishana twitter na kwenda kumtukana kwenye ukurasa wake wa instagram vitawasaidia...
 
Hao wakenya wanajitangaza wapi??

Kenge wewe watu wanatumia pesa na rasilimali watu kujitangaza sio kwenda twitter kuandika ujinga mpuuzi kabisa wewe...
Wewe huna Akili
Nahisi nimzigo ktk ukoo nasio familia kwa ujumla

Kila mwananchi anawajibu wa kuitangaza nchi yake

Na sio lazima kuitangaza mpaka kwenye mikutano ya kimataifa

Unapaswa ujue kujitangaza unaweza tumia njia yeyote
Muhimu njia ile itawafikia watu wengi
Hiyo twitter unajua idadi ya watu wanao itumia!!?

Jiulize kwanini miatandao yasimu inajitangaza kwenye runinga
Lakini pia hutumia hujitangaza kwenye mitandao ya kijamii.
JF Leo hapo juu kuna tangazo la voda kwanini liletwe hapo

Tatizo Akili zenu zimekaliwa na Misukule
 
Wewe huna Akili
Nahisi nimzigo ktk ukoo nasio familia kwa ujumla

Kila mwananchi anawajibu wa kuitangaza nchi yake

Na sio lazima kuitangaza mpaka kwenye mikutano ya kimataifa

Unapaswa ujue kujitangaza unaweza tumia njia yeyote
Muhimu njia ile itawafikia watu wengi
Hiyo twitter unajua idadi ya watu wanao itumia!!?

Jiulize miatandao yasimu inajitangaza kwenye runinga
Lakini hutumia hata mitanfao ya kijamii kuitangaza
JF Leo hapo juu kuna tangozo la voda kwanini liletwe hapo

Tatizo Akili zenu zimekaliwa na Misukule
Acha blah blah wewe kenge.. Kujitangaza twitter ndio kutaleta watalii?? Kenge mkubwa wewe alafu watu wenyewe ambao mnatangaza nchi ndio kama wewe Mtalii gani atakuja?? Hivi mnafikiri wazungu ni wapuuzi au??
 
Back
Top Bottom