Karibuni Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi

Karibuni Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi

Joined
Dec 23, 2017
Posts
35
Reaction score
69
Tarehe 25/8/2020 serikali imefungua maombi ya kuanza kuomba kujiunga katika vyuo vya ualimu kikiwemo PATANDI....

Kimsingi vyuo vyote vya ualimu vitaanza kutoa STASHAHADA baadala ya ASTASHAHADA hivyo kakauli rahisi ni kuwa hakuna tena ualimu ngazi ya cheti itakayotolewa na wizara..

SIFA ZA KUJIUNGA NA PATANDI
Sifa hizi zimegawanyika sehemu mbili walimu kazini na wale wasio walimu kazini kama ifuatavyo:-

i-Walimu kazini stashahada ya msingi
a)uwe na uzoefu wa miaka miwili kazini

b) uwe umepata ufaulu katika somo lolote la sayansi katika kidato cha nne
Muda wa kozi: miaka miwili

ii-Walimu kazini stashahada ya sekondari
a)uzoefu miaka miwili kazini

b)uwe na stashahada nyengine ya sekondari

c)uwe na ufaulu wa masomo ya sayansi katika kidato cha sita.

iii-walimu wasio kazini
a)uwe umemaliza kidato cha nne au kidato cha sita kati ya mwaka 2017 na 2018 tu

b)uwe umepata ufaulu kati ya daraja I - III kidato cha nne

c) uwe na ufaulu kwenye masomo ya sayansi na hisabati

d) cheti cha kidato cha sita ni sifa ya ziada

Kujiunga na na chuo cha ualimu patandi unaingia www.moe.go.tz unajaza fomu maalumu....
 
Hongera na Ahsante kwa taarifa murua kabisa tutawapa vijana taarifa.
Vip walimu walioko kazini na wana elimu ngazi ya cheti, hawawezi kuathirika na mabadiliko haya baadae.
 
Ada kwa mwaka bei gani?
Na hiyo Elimu maalum ni kwa walemavu wa aina zote?
 
Ada kwa mwaka bei gani?
Na hiyo Elimu maalum ni kwa walemavu wa aina zote?

Nafikiri upo sahihi, chuo ni kimoja tu hapa Tanzania lakini pana shule kiasi kidogo za watu hao wakati wahitaji wengi hawapati mafunzo hayo kutokana na hali halisi ya kutokujua wapi msaada unapatikana ikichangiwa na umaskini wetu
 
Back
Top Bottom