Karibu usome ushairi la 'Chozi la Mwana Ziwani

Yussufhaji

Member
Sep 9, 2018
35
28
CHOZI LA MWANA ZIWANI
Ngozi yote mesinyaa,
Nywele zote mesosoka
Chuchu zote mesinyaa,
Kwake amebahatika
Jasho linamhadaa,
Maziwa meshakatika
CHOZI LA MWANA ZIWANI,
NANI ATAELIONA

Maisha yalo dhalili,
Mwana chozi alitoa
Hana lile wala hili,
Kikohozi akohoa
Wake mustakabali,
Hapajui pakutoa
CHOZI LA MWANA ZIWANI,
NANI ATAELIONA

Mama apika andazi,
Usiku wa manane
Ayauza maandazi,
Asubuhi saa nne
Huo ndo wake ujuzi,
Hajali wake unene
CHOZI LA MWANA ZIWANI,
NANI ATAELIONA

Mchana unapofika,
Ugali ausokota
Ubwabwa tele kupika,
Auza kote tabata
Manispaa wafika,
Kutaka kumkamata
CHOZI LA MWANA ZIWANI,
NANI ATAELIONA

Faini kuja toleshwa,
Shilingi mia tabaki
Wapi sasa takopeshwa,
Moyoni meta haruki
Mwili autoa rushwa,
Kuihiliki mikiki
CHOZI LA MWANA ZIWANI,
NANI ATAELIONA

Na Jioni napoingia,
Azisakata chapati
Wateja kuwachungia,
Asibaki hati hati
Watoka na kuingia,
Kumtandika lo miti
CHOZI LA MWANA ZIWANI,
NANI ATAELIONA

Usiku kucha akesha,
Mwana kulitoa chozi
Hakuna to furahisha,
Ateseka wa azizi
Nani atawawezesha,
Maisha yao kuenzi?
CHOZI LA MWANA ZIWANI,
NANI ATAELIONA

Na
@Yosef_de_khuzhov
Fb: Tungo za Mtoto wa Mkulima
Youtube: Mtoto wa Mkulima
Email: hajjyussuf2@gmail.com
Simu: +255777158131

Adobe_Post_20200224_1459300.6198575225845274.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom