Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,383
KARIBU IJUMAA
1. Karibia ijumaa, twakusubiri kwa hamu,
Majizi yanasinyaa, katu hayanayo hamu,
Mafisadi kuyangoa, hiyo kwetu ni karamu,
Imefika ijumaa, tuone hatima yao.
2. Tutawavuta kwa kamba, tuwashike masikio,
Tuwatie jamba jamba, hadi kwenye machinjio,
Wamezoea kusomba, kila kitu kama chao,
Imefika ijumaa, tuone hatima yao.
3. Ijumaa imefika, twangojea uamuzi,
Moshi mweusi wafuka,tena bila ya ajizi,
Hakuna kusalimika, mafisadi ni kitanzi,
Imefika ijumaa, tuone hatima yao.
4. Shoka sasa li shinani, kukata lipo tayari,
Limeanza mitaani, kutanguliza habari,
Laendelea mwakani, wakizidisha jeuri,
Imefika ijumaa, tuone hatima yao.
5. Majizi yote pembeni, twaja mbio tupisheni,
Ofisi zetu acheni, m-pelekwe gerezani,
Fedha zetu rudisheni, kifungo chawangonjeni,
Imefika ijumaa, tuone hatima yao.
By Kitaja wa Jamii Forum.