Kariakoo: Machinga waondolewa mitaa yote ya katikati ya jiji

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,556
3,838
Wakuu kumekucha,

Napita katika mitaa ya Kariakoo, mitaa ni open, hali ya msongamano kama ilivyo kawaida haipo tena. Njia ni nyeupee

Watu wamekaa makundi makundi hawaamini kinachoonekana, hali ni tulivu hakuna vurugu wala kokoro, kumetua kimyaa. Wafanyabiashara wa Kariakoo wanashangilia mioyoni kwa hali hii.

Hongera kwa Manispaa, Hongera kwa Mkuu wa mkoaa #Vivaa umoja

BACK TANGANYIKA
 
Hongera kwa UKAWA sio Makonda, serikali ya ccm miaka zaidi ya 30 imeshindwa kutekeleza hilo, UKAWA ndani ya miezi 6 tu wameweza, ku deal na binadamu inahitaji busara sio ubabe, wamepewa maeneo yamewekwa miundo mbinu hakuna tatizo, sio ile fukuza fukuza ya zamani haioneshi waende wapi.
 
unafurahia watu kunyimwa ugali
TUKIENDEKEZA HIZI KAULI, HATUWEZI WAFIKIA HIZO NCHI MNAZO SEMA ZIMEENDELEA, Na kila siku tutasifia usafi wa nchi za wenzetu, hivi umeshawaza wale ambao wamelipa kodi ya frame au kodi eneo afanye biashara, halafu mtu anakuja kukaa mbele ya biashara yake anauza na kuziba kila kitu, tena wanaweka chini na humo humo msongamano usiokuwa na sabab ambao wale vibaka hupata nafasi ya kujifichia. NAONA UMEWAZA UPANDE MMOJA TU, SI LAZIMA SOTE TUWEPO MJINI, WENGINE TUKALIME MIWA SUKARI ISHAPOTEA.
 
Ukawa na Manispaa mmewapeleka wapi hao Machinga baada ya kuwaondoa?
Mkurugenzi wa jiji ndio alitoa hiyo habari ya kuhamisha machinga wote, madiwani wakapinga ila sasa hivi wamekubaliana kuwahamisha.Na kuna masoko yametengwa kwa ajili yao ila madiwani walisema hayo masoko hayana maji wala vyoo na miundombinu kwa ujumla ni mibovu.
 
Masoko yapi mkuuu ambayo yametengwa unawezaji kuwachukua watu 400 na kwenda kuwaweka sehemu moja wafanye biashara bila kuwawekea huduma za kibinadamu daah!
 
unafurahia watu kunyimwa ugali

Mkuu si kwamba nashangilia

Kama ni suala la Mkate wale kihalali, Kamwe hakuna nchi yoyote inayoruhusu kufanya biashara Barabarani. Tambua si lazima wote tukusanyike mjini kwaajili ya Biashara, wengine wanakimbia Kitabu kwasababu kunanjia ya mkato kama hizi za kufanyabiashara popote bila kujali lolote.

Kama umewahi kupita mitaa ya Kkoo hususani mitaa ya Congo, Nyamwezi, Aggrey na mingineyo utakuwa unaijua hali halisi ya mitaa hiyo. Watu wanapanga bidhaa barabarani hata kwa kukanyaga panakosekana. Ikitokea umekanyaga kwa bahati mbaya bidhaa hizo, kama kiganja au matusi ya nguoni basi utalazimishwa kununua kinguvu.

Ni mitaa hiyo hivi juzi wameua mfanyabiashara kwa kosa la kukanyaga mali zao kwa bahati mbaya. Mfanyabiashara huyo alikuwa na vielelezo vyote vya kufanyabiashara ikiwemo leseni na Mapato aliyolipa kwa miaka kadhaa aliyofanya biashara. Hao waliomuua ukiwaambia waonyeshe hata leseni tu hawana.

Napate nguvu ya kuwatetea watu hawa?

BACK TANGANYIKA
 
TUKIENDEKEZA HIZI KAULI, HATUWEZI WAFIKIA HIZO NCHI MNAZO SEMA ZIMEENDELEA, Na kila siku tutasifia usafi wa nchi za wenzetu, hivi umeshawaza wale ambao wamelipa kodi ya frame au kodi eneo afanye biashara, halafu mtu anakuja kukaa mbele ya biashara yake anauza na kuziba kila kitu, tena wanaweka chini na humo humo msongamano usiokuwa na sabab ambao wale vibaka hupata nafasi ya kujifichia. NAONA UMEWAZA UPANDE MMOJA TU, SI LAZIMA SOTE TUWEPO MJINI, WENGINE TUKALIME MIWA SUKARI ISHAPOTEA.

Sio lazima sote tuwepo mjini ,wengine tukalime miwa .....kauli za walioshiba hizi ,nini maana ya destiny na fate ??? Sio kila anayekaa hapo anapenda awe hapo ila imetokea ,badala ya kejeli ni bora walau tuwafariji ,
Oh nimekumbuka hakuna aliyeshiba anayemkumbuka mwenye njaa
 
Ukawa na Manispaa mmewapeleka wapi hao Machinga baada ya kuwaondoa?

Mkuu kuondoka kwa Machinga Kkoo ni makubaliano ya pande mbili zilizokuwa zinakinzana juu ya kuondoka kwa Machinga hao.

Makubaliano haya yamefanyika chini ya Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi kwa upande mmoja na Meya wa ilala na Baraza la Madiwani kwa Upande mwingine.

Kwahiyo urahisi wa swali lako unaweza kupata hata kwakumpigia Makonda.

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom