Karatu yataka Katiba isambazwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karatu yataka Katiba isambazwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jan 9, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  SERIKALI imeombwa kuhakikisha inatoa nakala nyingi za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuzisambaza kila kona ya nchi hii ili kila Mtanzania aweze kuisoma na kujua mapungufu yake.

  Ushauri huo umetolewa na wananchi wa mji wa Karatu katika Tarafa za Mbulumbulu, Endabash na Karatu, mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Therezya Huvisa aliyekuwa katika wilaya hiyo kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao juu ya mchakato wa uundwaji wa Katiba Mpya.

  Mkazi mmoja wa Tarafa ya Karatu aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Kingu, alisema hawezi kuchangia chochote juu ya Katiba mpya kwa sababu hata iliyopo haijui na wala hajawahi kuiona.

  Alisisitiza kuwa, itakuwa vigumu kwake kuchangia juu ya muundo wa Katiba Mpya na kuongeza kuwa, anaamini hayuko peke yake, bali Watanzania wengi hawaijui katiba iliyopo.

  Kutokana na hali hiyo, aliitaka serikali kuhakikisha Katiba iliyopo inawafikia Watanzania kote nchini ili waweze kuosoma na kujua mapungufu yake na kuongezea yaliyokuwa hayapo.

  Waziri Huvisa aliwashukuru wananchi hao kwa maoni yao mazuri na kueleza kuwa maoni yao atayafikisha kwa viongozi husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

  Alisema suala la kutolewa nakala nyingi za katiba ni suala muhimu sana hivyo basi atalifikisha kwa Waziri wa Sheria na Katiba ili liweze kufanyiwa kazi ipasavyo.
   
 2. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Tunaisubiria kwa hamu sana!hatuwezi changia chochote bila kufahamu kilichopo ndani ya katiba!unless hatuna haja nayo!
   
Loading...