Karandinga la polisi kupiga honi hovyo

PauliMasao

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2007
Posts
286
Reaction score
39
Hivi huu upumbavu wa karandinga la polisi kupita hapa mjini Arusha na kupiga honi kwa mfululizo bila dreva kujali madereva wengine na kuwasumbua wakazi wa jiji hili utaisha lini? Hili huwa linafanyika wakati mahabusu wanapelekwa mahakamani au wanapotoka kurudi magereza. Ni lini hawa polisi wataanza kusimamia sheria?
 
Mi hata sijui huwa wanakimbilia wapi na watuhumiwa wao. Jana nimeshuhudia kwa macho yangu huku Dar, cruiser na basi la magereza vikihama njia na kuingia kulia (along Kawawa road maeneo ya Msimbazi centre) kisa foleni ya kuingia boma. Swali ni walikuwa na haraka gani hadi kupita wrong way.
 
msilalamike that is for security reasons wanaogopa yasije yakatekwa wafungwa wakatoroshwa.
 
wapumbavu tu hao,walimgonga kijana mmoja mtembea kwa mguu hapa idara ya maji Arusha sijui kama alipona yule mtu,kilicho niuma ni yule dereva baada ya kumgonga yule mtu akawa anacheka.hii nchi upumavu mwingi unafanywa na walinda sheria ,yaani wale wasimamizi wa sheria ndio wavunjifu wakuu wa hiyo sheria wanayoisimamia
 
kila shughuli zina taratibu zake, hata ww ungekuwa upande wao, ungefanya kama wao wanavyofanya. gari hilo limebeba watuhumiwa wa uhalifu mbalimbali. hivyo tahadhali kubwa inatakiwa iwepo. ktk kuwapeleka , kuwarudisha na kuwalinda wakiwa mahakamani na gerezani pia. japo wanakuwa wakiendesha pasipo kufuata utaratibu wanapaswa kuwa na umakini mkubwa kwani ajali ikitokea sheria za usalama ziko palepale. hata madereva wanaokuwa barabarani wakiona magari hayo au ambulance ni vyema kuyasaidia kwa kupisha njia.
 
Mahabusu na wafungwa ni precious cargo. Waache honi watumie matarumbeta? Honi hizo zinaepusha utekaji nyara kwani eneo kubwa linakuwa linarindima.
 

ili jeshi la polisi lina mambo ya kutia aibu sana .hivi kweli wanakosa hela ya kununulia kingora cha polisi sh laki na nusu na taa za kimulili sh elfu 80 .shame on you tz polisi .tena polisi wanatakawi waelimishe madereva juu ya umuhimu wa kupisha gari za polisi,fire, na ambulance mara wasikiapo kingora .na pia kufanya mazoezi ya utayari wa kupishwa gari za polisi .ect.angalau kila baada ya miezi 3 ili kuwazoesha watumiaji barabara . Ni aibu sana kwa jeshi la karne 21 kushindwa ata kufanya kitu kilicho kuwa kinafanyika duniani kote kwenye karne ya 19 .MWEMA UNATIA AIBU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…