Kara-Murza mpinzani wa utawala wa Vladimir Putin yupo mahututi kwenye Coma kwa kulishwa sumu

mcomunisti halisi

Senior Member
Jan 17, 2017
103
328
Mwaka 2015 mwanaharakati na mpinzani wa utawala wa Putin kwa jina la Vladimir Kara-Murza (35yrs) alipata matatizo ya viungo vyake kufeli na kwa bahati nzuri aliweza kupona na kuishi baada ya kuwa kwenye Coma kwa takriban wiki nzima.Siku ya Alhamisi imemtokea tena hali hiyo tena kwa ufanano ule ule wa mwaka 2015.

Kara-Murza ni mwandishi wa habari wa zamani ambaye amefanya kazi katika kituo cha Russia Tv iliyopo Washington mpaka alipotimuliwa kazi mwaka 2012.Mwaka ambao Vladimir Kara Murza alitimuliwa kazi alitoa ushuhuda kuhusu ukamatwaji na utesaji wa Magnitsky ambaye alikuwa mwanasheria huko Urusi jambo lililosababisha Congress kuwawekea vikwazo vya kiuchumi na usafiri maofisa wa Urusi.Kara-Murza amekuwa mstari wa mbele kukosoa utawala wa Vladimir Putin uliojaa matendo mbali mbali ya uvunjifu wa haki za binaadamu.

kwa matendo ya Vladimir Kara-Murza hakika hakupendwa Kremlin na pia mahusiano yake ya ukaribu na Borisov Nemtsov ambaye ni mwanasiasa wa upinzani ambaye aliuliwa kwa kupigwa risasi wakati akielekea Kremlin february 2015 na miezi 3 baadae Kara-Murza alikuwa mahututi mara baada ya kula chakula chenye sumu katika moja ya mgahawa.Kara Murza Aliuambia kituo cha habari cha CNN kwamba ''Hakuna sababu nyingine yeyote ile zaidi ya siasa kwenye ulishwaji sumu huu.

Kara-Murza ambaye ametoa mchango kwa miaka mingi kuelezea jamii na kutahadharisha udikteta wa Vladimir Putin saizi anapigania maisha yake katika hospitali ya Moscow.Rafiki wa karibu wa Kara-Murza aitwaye Garry Kasparov alisema siku ya ijumaa wiki iliyopita ''utawala wa Putin unataka mabaya kwa wale wanaoitakia mema Urusi na Putin hana hofu ya kufanya matendo ya uuaji hata nje ya nchi na zaidi hata mambo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa amani.

Matendo ya ulishwaji sumu kwa wapinzani wa utawala wa urusi hufanyika mara nyingi matukio kadhaa ambayo yaliweza kufanywa na KGB huko nyuma ni tukio la ulishwaji sumu wa afisa wa zamani wa KGB Alexander Litvinenko ambaye alikuwa anaishi uhamishoni uingereza.Pia Rais wa zamani wa UKraine anakisiwa alilishwa sumu na KGB.ukiachana na kesi za ulishwaji sumu wapo waliouliwa kama mwanasheria Sergei Magnitsky na mwanasiasa wa upinzani Boris Nemtsov.

''Yupo katika hali mbaya ,vipimo vinaonyesha amewekewa sumu na kitu kisichojulikana.''-alisema mke wa Kara Murza

''Maabara nchini Ufaransa na Israel wanafanyia utafiti sample baada ya vipimo Urusi kuonyesha hakuna chochote.

''Mume wangu alitakiwa asafiri kwenda USA siku ambayo alizidiwa hali na kupelekwa hospitalini.''-alisema mke wa Kara Murza
''
Vladimir Kara Murza yupo mahututi saizi,yupo kwenye coma akipigania maisha yake,je safari hii atapona tena kama ilivyokuwa 2015?

Au safari hii KGB wameamua kummaliza mazima?


kara-murza-0.jpg
 
Inamaana Putin yupo hivyo?
Mi nahisi hao wanasiasa wanatumiwa na mataifa ya magharibi kuja kuihujumu Russia.
Ndio maana KGB wameamua kuwawahi mapema.
 
Back
Top Bottom