Mkuu Yahoo hawa jamaa wanavigezo vyao walivyotumia, lakini pia walikuwa na kategori mbalimbali, baadhi ya kategori ni kama zifuatazo: WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOCHEZA NJE:
Henry Joseph-Soka, Mbwana Samatta-Soka na Sophia Mwasikili-Soka-Samata alichukua; MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI: Theresia Ojode- wavu (Jeshi Stars), Shomari Kapombe- (soka) SIMBA na Salum Abubakari-Azam (soka)-hapa alipata tuzo hii Kapombe; MCHEZAJI WA NJE ANAYECHEZA TANZANIA:Haruna Niyonzima-Yanga (soka), Kipre Tchetche-Azam (soka) na Emmanuel Okwi-Simba (soka)-Okwi alichukua; SOKA (WANAWAKE):
Asha Rashid-Mburahati Queens, Mwanahamisi Omary-Mburahati Queens, Fatuma Mustapha-Sayari na Ito Mlenzi-JKT; WANAUME:
John Bocco-Azam, Aggrey Morris-Azam na Juma Kaseja-Simba-Aggrey Morris alichukua na mwisho pamoja na kategori zingine zote Kapombe aliibuka kidedea,
Kwa hiyo Kaseja asingeweza kuchukua tuzo ya jumla maana hata kwenye kategori aliyokuwepo bado hakubahatika kuchukua tuzo hiyo, all in all dogo ni mzuri na kingine kilichombeba ni uwezo wake wa kucheza namba nyingi uwanjani na nidhamu pia ndani na nje ya uwanja.