Kanusho la taarifa kuhusu UKIMWI kupimwa nyumba kwa nyumba

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,743
22,452
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazotokana na habari iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la tarehe 24 Juni, 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari "Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba".

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kutoa ufafanuzi kwamba UKIMWI HAUTAPIMWA NYUMBA KWA NYUMBA bali itafanya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania kuanzia mwezi Septemba 2016 ambapo UKIMWI utapimwa kwenye kaya chache ambazo zimechaguliwa kitaalam nchi nzima ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine nyingi ambazo hazitahusika moja kwa moja katika utafiti huu.

Utafiti huu utajumuisha kaya zipatazo 16,000 ambazo ni sampuli iliyochaguliwa kisayansi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na utahusisha watu wazima wasiopungua 40,000 wakiwemo watoto takribani 8,000.

Aidha, katika utafiti huu kutakuwa na kupima homa ya ini, kupima wingi wa chembechembe za damu yaani CD4, kupima wingi wa virusi katika damu na kupima kiwango cha ufanisi wa dawa za kufubaza VVU kwa watu wanaotumia dawa hizo.

Ifahamike kwamba, utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016 unafanyika nchini kwa mara ya 4 ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003, wa pili ulifanyika mwaka 2007 na wa tatu ulifanyika mwaka 2011.

Hivyo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inapenda kuwatoa hofu wananchi kwakuwa utafiti huu sio mpya katika nchi yetu na watanzania ambao wamekuwa wakipitiwa na utafiti huu, wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa zaidi ya asilimia 90.

Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya kwa Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Dar es Salaam,
28 Juni, 2016.
 
Hiyo Sample Yenu Ya Utafiti ya watu 40,000 kati ya watz elf 45 Wakubwa Wa Nchi Wataikataa Kwamba Haita Aksi Ukweli. Kumbuka Katiba Ya Warioba Ilikataliwa Kwa Sample Kama Hiyo. Vinginevyo Serikari Itakuwa Biased kama itawaruhusu kutumia hiyo sample..
 
Hapo sawa maana hili lingekuwa mojawapo La maajabu ya dunia. Yaani unipe ngoma kwa nguvu thubutu.
 
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazotokana na habari iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la tarehe 24 Juni, 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari 'Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba'.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kutoa ufafanuzi kwamba UKIMWI HAUTAPIMWA NYUMBA KWA NYUMBA
 
Sasa hizo kaya 16,000 wanazipata wapi Kama sio nyumba Kwa nyumba...???
 
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazotokana na habari iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la tarehe 24 Juni, 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari 'Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba'.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kutoa ufafanuzi kwamba UKIMWI HAUTAPIMWA NYUMBA KWA NYUMBA
Hautopimwa nyumba kwa nyumba illa ni kitu gani kitafanyika??
 
Point muhimu hapa ni kuwa participation should be voluntary...
Hakuna mtu atakaetolewa damu kama hataki kushiriki. Nafikiri hii ni point muhimu ambayo NBS wanatakiwa kuiongezea.
 
Wingi wa chembechembe za damu sio CD4!!!!CD4 ni protini-wanga ambayo ni aina tu ya chembe nyeupe za damu,inayosimamia mfumo wa kinga. Na kwenye VVU/YKIMWI haihitaji kupima wingi wa chembechembe za damu. Na kama wanataka kupima wingi wa damu, basi wapime hemoglobin.
 
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazotokana na habari iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la tarehe 24 Juni, 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari "Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba".

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kutoa ufafanuzi kwamba UKIMWI HAUTAPIMWA NYUMBA KWA NYUMBA bali itafanya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania kuanzia mwezi Septemba 2016 ambapo UKIMWI utapimwa kwenye kaya chache ambazo zimechaguliwa kitaalam nchi nzima ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine nyingi ambazo hazitahusika moja kwa moja katika utafiti huu.

Utafiti huu utajumuisha kaya zipatazo 16,000 ambazo ni sampuli iliyochaguliwa kisayansi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na utahusisha watu wazima wasiopungua 40,000 wakiwemo watoto takribani 8,000.

Aidha, katika utafiti huu kutakuwa na kupima homa ya ini, kupima wingi wa chembechembe za damu yaani CD4, kupima wingi wa virusi katika damu na kupima kiwango cha ufanisi wa dawa za kufubaza VVU kwa watu wanaotumia dawa hizo.

Ifahamike kwamba, utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016 unafanyika nchini kwa mara ya 4 ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003, wa pili ulifanyika mwaka 2007 na wa tatu ulifanyika mwaka 2011.

Hivyo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inapenda kuwatoa hofu wananchi kwakuwa utafiti huu sio mpya katika nchi yetu na watanzania ambao wamekuwa wakipitiwa na utafiti huu, wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa zaidi ya asilimia 90.

Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya kwa Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Dar es Salaam,
28 Juni, 2016.
Kama hawatatumia polisi hawampati mtu
 
Point muhimu hapa ni kuwa participation should be voluntary...
Hakuna mtu atakaetolewa damu kama hataki kushiriki. Nafikiri hii ni point muhimu ambayo NBS wanatakiwa kuiongezea.
Pongezi sana kwako mkuu
 
Back
Top Bottom