butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,769
- 8,260
TAFUTA MAARIFA
Biblia yasema watu wangu wameangamia kwa kukosa maarifa________________________ maarifa ndio yanayomtofautisha binadamu na wanyama wengine kuwa binadamu ana maarifa zaidi. Anaweza kurahisisha maisha yake. vitu vingi tunavyoviona sasa maishani ni matokeo ya binadamu kutafuta kuhodhi na kutumia maarifa. Waza kwa mfano; X-ray hospitalini, Daktari anavyopasua moyo, ubongo, n.k. meli meli zinazotuletea vitu toka sehemu mbalimbali, ndege zinazosafirisha watu angani, nguvu za umeme zinazotumika kutupatia mwanga, kuendesha viwanda, viyoyozi, kupikia n.k. simu za mkononi, television, n.k yote haya ni matokeo ya mkusanyiko na matumizi ya maarifa ya sanyansi. Mtoto mdogo hapo nyumbani anaweza akauliza maswali zaidi ya mia kwa siku kuhusu kitu chochote ndani katika juhudi ya kutafuta maarifa. Baba au Mama utaona mtoto ni msumbufu si kweli bali mtoto ni kiumbe chenye kufahamu na kutambua wajibu wake wa kutafuta maarifa. Wengi tunawakasirikia watoto wanapouliza maswali tusiyoweza kujibu nap engine tunawakemea hasa tukiwa mbele ya watu. Wengi tunafanya hivyo kwa aibu ya kushindwa kujibu maswali ambayo kwa umri wetu tulipaswa kuwa tunafahamu.
Ni wangapi tukiwa ndani tunajiuliza maswali ya msingi kama vile nini faida ya chakula ninchokula mwilin, ni kiasi gani kinatosha n.k. jinsi gani naweza kuendesha shughuli Fulani kwa ufanisi au faida, ni vipi madawa ninayokunywa yanafanya kazi mwilini, nini faida ya kinywaji ninachokunywa, n.k. wengi hatufanyi hivyo, tunafanya vitu kwa kuwa tumemuona fulani, jirani, ndugu, rafiki anafanya, n.k hatutafuti maarifa.Tunakwenda na mkondo wa mto bila kujua unatupeleka wapi nap engine tulipaswa sisi kuamrisha mkondo uende tunakotaka kwani watu mashuhuri wanaeleza kuwa nguvu za akili zetu ni kubwa, kila binadamu anapaswa kuamua anataka kwenda wapi na sio dunia au hali ikupeleke kule inakotaka.
Unawezaje kuimarisha hari iende unakotaka bila maarifa? Haiwezekani
Sio kweli kuwa hatutambui umuhimu wa maarifa katika kufanikisha maisha yetu, la hasha! Iweje mtu awe tayari kumgharimia mtoto wa miaka minne-mitano mamilioni ya fedha kwenye shule za awali? Kila kila mtu analitaka hilo mtoto wake awe mwenye uelewa mzuri wa masomo ya shuleni za tunajivunia sana kusema mwanangu anaongea kiingereza bado yuko chekeche, mwanangu alikuwa wa kwanza darasani n.k mwanagu /mwanagu /mwanagu! Je vipi wewe mwenyewe? Unajifanyia nini katika maisha yako ya kila siku kujiongezea maarifa? Ni mara ngapi umesikia kuna mafunzo, warisha, semina umeamka na kusema Yes! Na mimi lazima nijiongezee maarifa. Mara nyingi hasa kama mafunzo ni ya bure badala yake tunauliza Je kuna bahasha? swali baya kabisa maishani kwani kule anakosoma mwanao wanagawa bahasha? Si wewe unatafuta fedha kwa udi na uvumba, wakati mwingine unakopa au kuuza mali zako za kudumu ili mtoto asome? Je huko shule wanagawa nini kama sio maarifa? Iweje wewe unafikiria mwanao anapaswa kuwa na maarifa sana ila wewe hapana! Tunapenda kujiridhisha kuwa nitasoma ili nani akaniajiri; tunasoma ili tuajiriwe? Eehe! Na yule mtoto kinda wa chekechea yeye anaajiriwa wapi? Kuna kampuni au ofisi inaajiri chehechea? Jiulize na ujibu lakini najua hakuna. Je mitaala ya shule za awali inafundisha ujasiriamali? Mototo anaenda shule ya awali ili ajifahamu, afahamu mazingira, afahamu lugha au mawasiliano, haya ndio maarifa anahitaji mtoto kujimudu.
Rafiki yangu aliwahi kuniuliza swali lililonifungua macho mwaka 1993, kwa nini nyiemlitoka kazini swali kubwa ni tukutane wapi leo jioni kwa ajili ya kunywa pombe? hamna kitu kingine cha kuwajenga mnachoweza kufanya jioni isipokuwa pombe? Nilimsikiliza kwa makini na nikatafakari. Ndio mzungu huyu ni boss, ana mshahara usiokatwa kodi elfu kumi kwa mwezi, halipii chochote anapofanya kazi hapa Tanzania zaidi ya chakula na mahitaji yam engine ya ndani. Analipiwa pango, usafiri, mawasiliano, likizo, ada za watoto n.k. mmi nina mshahara wa dola 200 lakini nashinda jioni kwenye baa kukata kinywaji. Anaendelea kuhoji mzungu huyo boss kuwa na watu wengi wanaokuja kuomba kazi wanashindwa usaili kwa sababu eti wanasahau mambo ambayo walisoma shuleni kwani ni miaka mimgi iliyopita wengine haizidi hata miaka mitatu. Akaendelea kushangaa na kuna faida gani kusoma shule zaidi ya miaka kumi na tano mpaka ishirini na kusahau yote ndani ya miaka mitatu? Akamalizia kwa kusema tatizo lenu ni kuwa mnasoma lili kupata kazi tu na mkipata mnatupa mtaji uliowafikisha kazini.wakeza katika elimu hata baada ya kumaliza shule kwani maarifa yanapaswa kufafutwa katika uhai wote wa mwanadamu na sio wakati uko darasani tu.
Hasara za kutotafuta maarifa ni nyingi sana sehemu kubwa ndio kisababishi kikubwa cha umaskini, matatizo ya kiafya, mahusiano mabaya, utendaji kazi hafifu (usio na tija) na ufujaji wa mali.
VYANZO VYA MAARIFA
Chanzo kikubwa cha maarifa ni ndani ya familia, mtoto anapozaliwa na kukua kufuata yale ambayo wazazi au na ndugu zake wanafanya. Ili kuongea lugha wanayoongea wazazi mtoto mdogo haendi darasani, anasikia na kuona wanazunguka wanavyofanya na kuwasiliana, huiga. Tunapaswa kuelewa kuwa chanzo kikubwa cha maarifa na wakati wote kinasahaulika ni jinsi familia inavyoishi hapo jumbani ni vitu gani vinafavywa ili kuongeza maarifa ambavyo mtoto anaona na anatamani naye kama vile wazazi wanavyofanya.
Je mimi mzazi ninayetoka kazini na kwenda baa au mtaani kunywa kahawa jioni yote au kucheza pool ni maarifa gani ninayomfundisha mtoto? Kwa taarifa yako, watu tunakumbuka sana vitu/hadithi au chochote ambacho tulisoma tukiwa wadogo kwa wakati wetu kuliko vile vya darasani. Jiangalie je ndani unavitabu vingapi vya aina gani ambavyo mtoto anaweza kunyanyua na kutamani kusoma kwani ameona mzazi unakisoma? Yawezekana majibu ni hapana, hivyo una shauriwa kuifuata kanuni ya kwanza ya maisha kuwa:-
ª Tambua kuwa chanzo kikubwa cha mafanikio maishani ni kuwa na maarifa, maarifa yanayotumika vizuri hivyo tenga muda katika masaa 24, siku 7 ulizopewa na Mungu kutafuta maarifa.
ª Iwe mwiko kusema napoteza muda aliopanga Mungu, mwiko kabisa.
ª Chagua vipindi vinavyojenga katika redio, televisheni na intenenti. Usiwashe TV kwa kuwa inawaka na kuonyesha, washa kwa kuwa kuna kitu unatafuta, TV ni sumu kwa vijana kwani asilimia zaidi ya sabini ya muda wa TV ni filamu za kuigiza, napigia mstari neno kuigiza nikiimanisha si vya kweli ni vya uongo. Kwa nini basi tunapoteza muda mwingi kuangalia vitu vya uongo wakati tugeweza kutumia muda huo kujifunza vitu vya kweli?
ª Watu wengi nasikitika kusema wametekwa na mchezo wa mpira hasa ligi za Uingereza na Hispania, unaweza kukuta watu wazima wanatumia zaidi ya masaa 3 kuangalia mpira nap engine saa 1 au zaidi kubishana. Tufahamu kuwa mpira ni mchezo, napigia mstari neno mchezo nikimaanisha kwa nini upoteze muda mwingi kwenye mambo ya mchezo? Unafahamu ya kuwa wanaowekeza kwenye mpira haja yao sio magoli wala chenga za akina Drogba, Ronald, Messi n.k. ni matangazo ambayo wewe unayaona na kukushawishi kununua bidhaa wanauza kuta za uwanja vifaa vya wachezaji n.k. si kwamba wao ni wapenzi wa mpira kwani hicho la hesha. Ungekuwa ni upenzi basi wangeenda kusaidia mpira mashuleni au timu za nchi maskini. Uwe mwangalifu sana kutumia muda mwingi kwenye suala la mchezo tu.
Tufunge somo hili kwa kusema, maarifa ndio ufunguo wa maisha bora, maarifa hutafutwa muda wote wa maisha ya binadamu tangu anazaliwa mpaka anapokufa.
Azimio lako binafsi liwe kuanzia sasa nitatumia masaa______________ kujisomea/kusoma kila siku au kila wiki siku za___________ mambo ambayo ningependa sana kujisomea ni yale yanayohusu
. .
.
Maarifa juu ya suala hilo nitayapata toka