mke wangu wa miaka 5,watoto 3 moja alikuja nae juzi kati kaniumiza sana kidogo ningepoteza jicho.. alingia kwenye facebook yangu akasoma msg zote zingine za nyuma kabla sijaanza kuishi nae.. baada ya kuisoma kupitia computer ya nyumbani nikiwa sikulog off, akaanza kunitumia msg za matusi.. nilijibu moja tu kwa kumwambia si nzuri kunitumia msg design hiyo.. nilivyorudi nyumbani nikiwa nimelala sofani..akanirushia sim jichoni kidogo angenitobolea jicho kabisa.. nikaanza kulia kwa maumivu...na akafunga mulango kabisa nilivyotoka nje.. nilifanikiwa kuchukua piikipiki kunipeleka kupata matibabu.. cha ajabu akanifuata hospitalini na akawa anaendelea na maneno yake.. watu walimshangaa sana.. ila nilikataa kurudi nae nyumbani na kulala kwa jamaa yangu.. asubuhi akaamuka akiwa anajua siwezi kwenda kazini kotokana na maumivu yangu akaenda mwenywewe na badala ya kutoa tarifa nzuri akaandika barua ndefu kunianika kwa boss wangu kwa lengo la kunifukuzia kazini.. kwa bahati nzuri secretari hakufikisha ile barua.. mambo yote ya ndani aliandika.. now ananiomba msamaha nifanyaje jmni?
Kwanza inaonekana hujui ulioa ili nini na hata hujui mke anapaswa aweje,usichukie nitakupa sababu .....
Huyo mkeo hana sifa ya kuitwa mke kwasababu mke anapaswa kuwa ni wa kupunguza matatizo na sio kuyaongeza kama huyo wako,lakini kingine zaidi ambacho ni cha ajabu ni yeye kushindwa kujua kazi un ayoifanya sio yako tu bali ni yenu,hajui kabisa yeye ni nani na nafasi yake kwako na kwenye ndoa yenu ni ipi
Kwa hayo machahce tu umeshindwa kuyajua hii inaonesha kuwa hata wewe kufikiri kwako kuna tatizo,ila nadhani kuanzia sasa utajua,kwasababu hiyo basi ndio maana umeshindwa kujua hata cha kufanya na umekuja hapa kuomba ushahuri
Kimsingi thamani ya ndoa yako na umuhimu wa mke kwako na kwa familia yako ilitakiwa uanze kuona wewe lakini pia mtu hatari kwenye familia yako ulitakiwa uanze kumuoa wewe kama baba wa familia kwasababu baba ndie muangalizi wa familia na msimamizi pia,yaani baba ndie ambae anahakikisha usalama kwenye familia yake,ukilegalega familia yako inaingia matatani na ndiop hiki ambacho kinatakakuifuata familia yako
Lakini nakupongeza kwa kujua kuna tatizo hadi umekuja kuomba ushauri hapa,hii ni njia nzuri japokuwa imeonesha udhaifu fulani kwako,udhaifu sio kuomba ushauri bali ni kitendo cha wewe kushindwa kuyaona makosa ya kawaida kama haya
Kimsingi unachopaswa kufikiri sasa ni kama uliingia kwenye ndoa ili upoteze furaha au laa,ukishapata jibu amua cha kufanya .......
By the way,hukutakiwa kulia mbele ya mkeo kabisa kijana,mwanaume unalia mbele ya mkeo kweli?