Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,892
Hapa nazidi kushangaa na kuprove kuwa binadamu mapungufu ni mengi na hatujakamilika kiukweli kweli.
Ukimsikia askofu Munga wa KKKT, Pia askofu wa Morovian, na wengine wachache unapata faraja kuwa wako na watu hao wanaonekana wachache na wanyonge katika kutetea haki za raia wasio na sauti na wakiwasemea.
Lakini jana nimeshangaa kanisa kongwe kuungana na serikali kikandamiza haki za watanzania.
Hawa viongozi wa dini na sio wa kiroho walichokishuhudia kwenye chaguzi za mitaa wakati wa zoezi la uandikishaji, uchukuaji na urejeshaji wa fomu walitaka vyama vya upinzani wafanye nini ikiwa 96% ya wagombea walienguliwa? Wakae meza moja meza ipi?
Dini ipo kwa kisudi la haki. Je kuna haki katika mchakato huu?
Hivi mnafikiri waumini wenu wasipoipata haki huko makanisani watakuja kufanya nini? Mnaongoza watu kiroho au kimaslahi ya kiserikali.
Mbona kipindi cha Kikwete mlikuwa huru na wazi kukosoa kwa Magufuli mna hofu ya ukatoliki wake?
Na kwa kauli ya jana mbona sijasikia ule msemo pendwa ya Kaisari mwachieni Kaisari na ya Mungu aachiwe Mungu.
Msemo huu huja pindi tu serikali imeonywa na kauli mbiu vueni majoho wapande kwenye majukwaa.
Ila kwa kauli hii safi kabisa.
Nilikumbushe kanisa toka mwanzo na historia ya dini iko wazi hakuna mtakatifu wala mtume anayejulikana kwa kuwa pamoja na serikali kwa sababu watu hao walitaka haki toka kwa watawala na neno la Mungu ni mwanga wa haki ambayo binadamu huinyima na kujimilikisha