Ni kiri wazi mimi nina imani kali sana unapozungumzia Mungu au Yesu kristo, Ni moja kati ya watu ninaoamini Mungu yupo na sisi sote ni mali yake.
Lakini taratibu nimeanza kuwa mtoro kanisani, si kwamba siombi Mungu. Hapana, Namwomba Mungu lakini nikiwa nyumbani au popote nitembeapo kimya kimya.
Kwanini nasema imani yangu imeporomoka juu ya makanisa. Nimeshuudia viongozi wa dini wakila kuku ikulu huku wakiambiwa na Rais mikutano ya ndani haijakatazwa nao wakashangilia bila ku challenge chochote, Huku chadema wakiwa wamekatazwa kufanya mikutano yao ya ndani mara nyingi na Ccm wakiifanya kila uchwao tena mpaka ya adhara.
Hili viongozi wahubiri haki hawalioni, Mtakumbuka Rais mara kadhaa ametuambia mikutano ya ndani ni ruksa lakini imebaki ruksa ya mdomo, Pale vyama pinzani wakitaka kuifanya inasambaratishwa.
Hawa viongozi wa dini hawaoni? Nini kimewapofusha kiasi kikubwa namna hii, Maandiko yamebadilika? Leo nimeshuudia ACT wakinyimwa kufanya mkutano wao wa ndani, Tena kwa sababu dhaifu mno aliyoitoa mambosasa. Lakini Lipumba na ndugai wakiwa na mikutano aina hiyo hiyo ikipatiwa baraka zote na polisi.
Hizi ndimi mbili na ukimya juu ya dhuluma na ubaguzi ukiendelea, kwa viongozi wangu wa dini.Nimalizapo kwaresma na kanisa kwangu litakuwa bye bye. Nitalipinga hata kwa maombi.”
Nitaendelea kumwomba Mungu wangu bila kwenda kuwasikikiza Mapadri au Maaskofu wasioweza kukemea dhuluma na kutete haki za waamini.
Na hili sio kwangu tu, Kanisa lisipo badilika yatabaki kama makumbusho kama huko ulaya, Au watabaki vikongwe tu.
Ni Yesu yupi mnamuhubiri kama yote yatendekayo hamyaoni?
Hivi dhambi ni kuzini tu? Badilikeni kabla waamini hawajabadilika.