ujanani nilikutana na jambo kama hili Kyela wakati tukifanya magendo ya power namba moja na sukari pori kwa pori na akina X ambaye kwasasa ni mbunge wa jimbo flani ndani ya mbeya na ni maarufu kwa biashara ya vipodozi,sasa pale nilikutana na dada ambaye kiukweli naweza sema ni moja kati ya wanawake waliowahi kunipenda sana aisee ndipo akaniomba nizae nae mtoto ili hata siku nikiondoka awe ana mtu wa kumfanya anikumbuke na alikuwa anajiweza kifedha na alisema kuhusu malezi atalea mwenyewe mwanzo nilikataa ila baadae niliingia mkenge nikakubali,mamvo yalienda sawa akabahatika kujifungua mtoto wa kiume na hapa ndipo kero zikaanza aisee yan nilikuwa mhuni asiye na mke lakini kichwa kilikuwa kinawaka moto sasa wewe mwenye ndoa itakuaje kama mambo yakija kupinduka,ilifikia kipindi kero zikazidi hadi nikabadili hata route ya biashara nkaanza kuingia malawi kupitia mto flani upo pale pemba karibia na tunduma,nilikuwa nimepanga pale Migombani ila alipeleleza mpaka akapajua na kwa kero zake ilibidi nihame pale wakat palikuwa ni muhimu sana strategically kwa shughuli zangu maana ni karibu na Mpaka wa Nakonde na pia palikuwa karibu sana na tazara/reli pia kuhama migombani kuninighalimu sana sana maana kipindi magendo yalipokuwa magumu(kuna kipindi dolia ya askar wa kuzuia magendo ilikuwa kali sana) nilikuwa nafanya biashara ya viatu ambavyo nilikuwa nachukua pale mwanjerwa au sido kisha napeleka Zambia Ndola na nilikuwa sometimes napata faida ambayo kuna muda nilitaka hata niachane na magendo,hii biashara ilibidi niiue kwa kero za yule bibie nikaludi iringa
Na mbaya zaidi niliwah kumwambia kijiji nachotokea(ndani ya iringa)aisee kuna siku sina hili wala lile nilimkuta nyumbani kwa mzee wangu kaleta mtoto....ni hadithi ndefu sana ila nilisusiwa mtoto ambaye kwa sasa ni mtu mzima sasa
Kataa hiyo kitu kwa faida yako,familia yako na hiyo ndoa yako yenye fulaha ndgu yangu