nkungu mwere
JF-Expert Member
- Sep 6, 2018
- 258
- 336
Si mchambuzi mahiri wa soka,lkn napenda kuchambua matatizo,sababu,na njia ya kufanya pengine tutoke tuliko kwama,ili tufanikiwe katika soka lazima tuwe na wachezaji wenye vipaji,na pia tuwe na viongozi wenye kujua kuongoza mpira (narudia kuongoza mpira)na sio mtu kuwa mchambuzi mahiri wa mpira basi naye anajua kuongoza,pia tusichanganye siasa na mpira(hasa ikitokea wengi hawaipendi aina ya hiyo siasa)nianze na viongozi,wengi wanaoitwa viongozi hasa kwenye vilabu na huko TFF sio viongozi sahihi wa kuvifanya vipaji tulivyonavyo vikue na hatimaye vitusaidie siku za usoni(hii ni kwa kuwa vipaji vipo tele)tuangazie ushiriki wa timu zetu 4 ktk michuano ya CAF mwakani,ukosefu wa mipango ya muda mfupi na mrefu wa viongozi wetu umetufanya tukose waalimu wazalendo wa kufundisha timu zetu,AZAM,SIMBA,YANGA,KMC,zote waalimu wanatoka nje,tena wengi ni majirani zetu,RWANDA,UGANDA,DRC,hii maana yake ni kuwa uongozi wa juu hauna uwezo wa kutufanya tuwe na makocha wazalendo bora au tusiwaamini makocha wazawa,kwa kukosa viongozi bora tumezalisha viongozi wa vilabu wasio na mipango ya muda mfupi wala muda mrefu,mfano viongozi wa simba,timu iliyojengwa kwa miaka miwili inakuja vunjwa na kusajili upya nusu ya kikosi,tena kikosi kizima cha SIMBA au YANGA hakuna mchezaji mwenye mkataba wa miaka mitano,ni miwili au mitatu, au mmoja,maana yake ni kuwa kila mwaka lazima tusajili upya au tufanye zoezi la mikataba upya,viongozi wenye malengo ya muda mrefu hutengeneza timu ya muda mrefu,sio timu ya msimu mmoja,pia usajili hufanywa kwa kukomoa wala si kwa mahitaji maalumuTAMBWE katemwa simba dakika kadhaa yanga wameshamtwaa,unajiuliza ni mipango ya benchi la ufundi au ni viongozi,NIYONZIMA kadengua yanga mara simba wanaye,ni mipango au umbumbumbu wa viongozi?unasajili chipukizi kama SALAMBA kesho yake unamletea KAGERE si kuua kipaji cha mtu huko,matokeo tumewapoteza chipukizi wengi kama mwashiuya,mhilu,salamba,kaheza nk,kuhusu TAIFA STAR unategemea timu bora ya taifa kutoka wapi,iwapo beki bora wa ligi anatoka zimbambwe,kiungo bora anatoka zambia,winga bora uganda,mfungaji bora rwanda,congo,kasoro kipa tu manula,bado tunamlaumu kocha,kujua hilo hebu fikiria hili,kipindi hiki ni cha usajili,umesikia wapi mchezaji wa kitanzania akigombewa na majirani zetu kama ambavyo tunagombea wachezaji wa majirani zetu?ikiwa hatuwezi kuuza wachezaji nje tutegemee nini,maana yake hatutengenezi wachezaji kama majirani zetu wanavyo fanya,na hata hao wawili watatu waliosajiliwa nje ni majirani ndio wamegundua vipaji vyao wala sisi hatukuvijua,ndio maana tunabaki kushangaa AMBOKILE akienda MAZEMBE timu bora afrika lkn si MO wala MSOLWA aliyemwona,mpira ni hesabu mpira sio papara,leo wako viongozi wanaotamani SAMATA aende uingereza ni kweli,lkn hesabu hii ni muhimu,heshima ya mchezaji yeyote ni kushiriki mashindano makubwa duniani,leo timu samata imefanikiwa kupata tiketi,lkn samata huyo huyo anatakiwa na timu isiyoshiriki ligi ya mabingwa kama EVERTON,lazima afikirie mara kumikumi,aende uingereza ligi bora lkn asishiriki ligi ya mabingwa,au abaki GENK ashiriki ligi ya mabingwa?hilo ndilo linakaribia kumkuta beki mpya wa yanga ALLY ALLY,kmc inashiriki afrika na alikuuwa na namba ya uhakiika,lkn ameenda yanga kugombea namba,ni dhahiri angebaki KMC angeuzika ki urahisi AFRIKA kuliko kwenda kubahatisha namba yanga,,,,,leo hii YANGA,AZAM,SIMBA,KMC,wanawalipa makocha wao pesa mingi ili wawatengenezee majirani wachezaji bora wa kutufunga,kwa kuwa kati ya hizo timu hakuna Itakayowaweka wageni bench ichezeshe wazawa.