Kanda ya Ziwa kukosa umeme siku 23

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Monica Petro
SHIRIKA la umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza kuwepo kwa mgao wa umeme siku 23 katika mikoa sita ya Kanda ya Ziwa na baadhi ya mikoa kutokana na mitambo ya umeme mkoani Singida kuzimwa.

Taarifa iliyotolewa na Meneja wa Mawasiliano wa Tanesco Badra Masoud alisema mikoa hiyo itakosa umeme kutokana na matengenezo ya mitambo iliyoharibika na kwamba itazimwa kuanzia Mei 23 hadi Juni 16, mwaka huu.
Mikoa hiyo ni pamoja na Shinyanga, Mwanza, Mara, Dodoma Singida pamoja na Tabora.
“Mikoa hiyo itakosa umeme muda wa siku nzima ili kutengeza mitambo na kuboresha umeme kutoka gridi ya ya taifa,”anasema taarifa hiyo.

Mgao huo unatatrajia kuanza mei 16 mwaka huu utakaoanza saa mbili asubui hadi saa kumi na moja jioni kwa msongo wa kilovati 220.
Alisema pia Mei 30 hadi Juni 6 kituo cha kupooza na kusafisha umeme cha Singida mitambo yake itazimwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku.

Wakati huohuo, mtambo wa pangani unaotumia njia ya kilovati 132 utazimwa Mei 18 na hivyo kutokuwepo kwa huduma ya umeme Manispaa ya Tanga.


Kanda ya Ziwa kukosa umeme siku 23
 
Back
Top Bottom