Kamuulize Kikwete

BAK na wewe nikuulize hii issue imeishia wapi au nayo ishapita ni kelele tuu hazimuamshi mwenye nyumba
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Akimaliza kuugulia msiba wa Bi mkubwa ataleta report kamili. Dogo ni jembe kweli kweli.
 
Zito anajua dili zima ajitokeze kueleza. Kumbuka mwizi hujifanya mwaminifu
 
Mkuu Rocky kama kawaida ya hii Serikali dhalimu inaendeleza kufanya usanii kwamba uchunguzi unaendelea huku hizo pesa zikiwa zinapungua kwa kasi ya kutisha. Mafisadi wahusika wameshazichota shilingi 35.9 billion kati ya karibu bilioni 328 zilizokuwepo awali ( Taarifa za 2011 kutoka Uswisi zilionyesha kuwa kuna kiasi cha Sh327.9 bilioni zilizofichwa kwenye benki za nchi hiyo, lakini Ripoti mpya ya mwaka 2012 ya Benki za Uswisi inaonyesha kuwa fedha hizo zimepungua hadi Sh291.96 bilioni.) Wakati uchunguzi wa pesa za wizi ukiendelea wahusika wameachwa huru wakiendelea kuchukua pesa hizo!!!!! Wanajiamini nini hawa mpaka waweze kufanya hivyo!? Sijasikia mahali popote duniani pesa ambazo ziko bank na zinashukiwa ni za wizi zikaachwa zichukuliwe na watuhumiwa. Tusishangae mwakani tukasikia mabilioni yote hayo yameyeyuka. Rais wa nchi kimyaaaaaa "hayamhusu"

Kesi tano za mabilioni Uswisi zachunguzwa - Kitaifa - mwananchi.co.tz

BAK na wewe nikuulize hii issue imeishia wapi au nayo ishapita ni kelele tuu hazimuamshi mwenye nyumba
 
Mkuu BAK mambo mengine Tanzania yetu hii wanasema ni upepo tuu utapita na unapita kimya kimya hakuna wa kuulizia maana wapiga filimbi ndio hao hao wanaochagua wimbo
Sasa ukishaona kesi ya Kurwa anapelekewa Doto jua hapo hakuna haki maana Kurwa hawezi kumuangusha ndugu yake Doto hata siku moja na watafanya kila njia kulindana
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Shida hata walioibiwa nao wamesahau kuulizia walioiba ndio wakumbushie mbona mtuulizi tena?
 

Mwakani wakati nyie mnaambiwa kuwa mabillioni yote yameyeyuka yeye ataku Msoga anafuga n'gombe wake na kumfanyia promotion Diamond; mafisadi wote wenye kesi na waliomagerezani watakuwa wamepewa msamaha wa rais na hivyo upepo utakuwa umepita!!! Bongo tambaraleeeee.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…