Ngoja nielezee kwa kitalaamu kipengele cha tatu. kwenye mfumo wa kibepari na kampuni za binafsi pesa yeyote inayotumika kwa mikopo au ujenzi n.k imetoka kwa mwekezaji. Mwekezaji hivyo inategemea kupata faida kutoka kwenye pesa yake aliyotoa.Kwa kampuni zenye hisa wawekezaji ni wenye hisa. Hii hapa ni njia (formular wanayotumia wawekezaji)
Required Rate of Retun = Risk Free Rate + Risk Premium
Maana yake ni kwamba kama mwekezaji anataka 7% (Risk Premium) kwa mwaka na serikali inauza T-Bond zake asilimia 10% (Risk Free Rate) kwa mwaka basi Mwekezaji anahitaji asilimia 17% ili aweze kutoa mkopo. Kama serikali itaongeza T-Bond kutoka 10% mfano mpaka 15% basi mwekezaji atahitaji asilimia 22% ili aweze kuwekeza. Hii ni kwasababu huwezi kupata mwekezaji anayehitaji asilimia 15% maana anaweza kwenda kununua T-Bond ambazo hazina risk na kumvutia ni lazima utoe zaidi.
Nitakuwa naendelea kutoa somo polepole ili nisiache watu.
Mkuu mi binafsi nashukuru sana kwa hili darasa, na pia naomba unieleweshe kidogo, Hivi Hizi T-Bonds zina masharti ghani kununuliwa,namaanisha kununua T-Bond moja kwa moja toka serikalini kwa mtu binafsi, Au ni mabenki tu na those big investors ndo wanasifa za kuzinunua?Say nina 50mil nataka niuzie serikali for a certain maturity period bonds,inawezekana?
So, endapo serikali ingepunguza viwango vya riba inazotowa kwenye dhamana zake, then government bonds zingepunguwa kuwa attractive investments kwa commercial banks, as a results, commercial banks zingetafuta alternative way of earning interests....na hapo ndipo zingegeukia upande wa commercial loans!
"pia itaendelea kutoa vitambulishio vya Taifa ambavyo kwa sasa vina taarifa zote muhimu za mwananchi,"
Sikulaumu kama umepiga kambi TZ na hujawahi kuishi dunia ya kwanza utashangaa lakini vitambulisho ni sehemu humimu sana na mikopo. Jitahidi kujifunza kutoka nchi nyingine hata kama haujafanikiwa kutoka TZ. Kuna wasomi wengi sana hawawezi kusaidia nchi kwasababu ya ushamba tu hivyo sikushangaieti vitambulisho vya taifa vina taarifa zote muhimu za mwananchi.
ni taarifa gani muhimu inayohusiana na mkopo inayoweza kuwekwa kwenye kitambulisho, kwamba unamiliki nyumba ndogo Mbande kwa bi. Kidawa?
Yunus hiyo system ya grameen ameiiga FINCA ndio wanayoitumiaMimi naamini kama benki zetu ama ingepatkana benk kama GRAMEEN inayoongozwa na Prof. Mohammed Yunus,watu maskini na hasa wa vijijini wangepata ukombozi. Mkulu aliwahi mualika huyu jamaa hapa tz,sijui ilikuwa ni upepo tu ukapita?