Kampuni hii ya Kimarekani ambayo imekuwa ikikiuka order za serikali na kung'ang'ania vitalu vya uwindaji sasa inazua maswali mengi. Mwaka uliopita gari moja ya kampuni ya Wengert Windrose Safaris ilikamatwa huko Arusha ikiwa na shehena ya bangi.
Mtuhumiwa hadi hivi leo hajafikishwa mahakamani licha ya kukamatwa red-handed akiwa na bangi kama inavyoonekana pichani. Inadaiwa kuwa wahusika wakuu wa mzigo huo hawajakamatwa hadi leo.
Nani anawalinda wahalifu hawa? Je, hiyo ndio sababu ya kung'ang'ania vitalu, ili kuendeleza biashara ya bangi?
Hawa watu kinachoshangaza ni kwa namna gani wanaweza kufanya jambo lolote walitakalo huku wakijua kwamba si sahihi. Haiyumkiniki kwenda Marekani na kufanya mambo ya kihuni ambayo serikali ya nchi hiyo haikubaliani nayo kisheria, kanuni au taratibu. Kwa nini vyombo vyetu vya dola havichukui hatua stahiki dhidi ya genge hili? nani anawalinda? Ana nguvu gani dhidi ya serikali yote ya Tanzania?
Nasikitika tu Tembo wetu ,miaka 20 ijayo itabidi nimwonyeshe mwanangu picha ya Tembo ,akiniuliza ulikua wapi kuzuia jambo hili lisitokee sijui nitamjibu nini ,bangi sina tatizo nayo hiyo kitu hata kwenye barafu inaota