Kampuni ya Rifaro Africa yafungiwa na TCRA, yatozwa faini!

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,786
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
ISO 9001:2008 CERTIFIED

TAARIFA KWA UMMA

KUTUMIKA RASILIMALI NAMBA MAALUMU 15420 NA KAMPUNI YA RIFARO BILA CHETI CHA MATUMIZI YA NAMBA CHA MAMLAKA YA MAWASILIANO

1.0 UTANGULIZI

1.1. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni taasisi ya Serikali yenye jukumu la kusimamia huduma za Sekta ya Mawasiliano na Utangazaji nchini, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa rasilimali namba kwa mawasiliano na anwani kuhakikisha matumizi sahihi.

1.2. Katika siku za hivi karibuni, Mamlaka imeona taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu Kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano. Yafuatayo ni maelezo ya Mamlaka kuhusu taarifa hizo:

1.3.Mnamo tarehe 28 Julai, 2014 Mamlaka ilitoa kwa RIFARO AFRICA LIMITED Cheti cha Matumizi ya Rasilimali Masafa kwa ajili ya huduma za ziada za Mawasiliano kupitia SMS (VAS SMS CODE) namba maalumu 15420 kutumika katika kutengeneza mfumo wa Mawasiliano wa SMS kuunganisha na kupokea taarifa za mawakala wao wa kuuza na kusambaza muda wa maongezi kupitia wavuti yao (website);

1.4.Mnamo tarehe 27 Julai, 2015 Cheti hicho kilimalizika muda wake na Kampuni ya RIFARO Africa Limited haikuomba kuongeza muda wa matumizi wa rasilimali namba maalumu 15420. Kuendelea kutumia rasilimali namba hiyo bila cheti cha kuruhusu kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano ni ukiukwaji wa Kanuni ya 17 (1) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 - Matumizi ya Namba na Anwani za Mawasiliano - (Electronic Communication Numbering and Addressing) Regulations, 2011.

2.0 AMRI YA UTEKELEZAJI

Mnamo tarehe 24th Februari, 2016, Mamlaka ilitoa Amri ya Utekelezaji kwa kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED kwa mujibu wa Kifungu cha 45 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania sura ya 172 kama ilivyorekebishwa na Kifungu cha 179 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta, na kuimauru kampuni hiyo kufika mbele ya Mamlaka ya Mawasiliano kujitetea kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kuvunja na kukiuka Kanuni namba 17 (1) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2011 - Matumizi ya Namba na Anwani za Mawasiliano kwa kutumia rasilimali namba maalumu 15420 bila Cheti cha kuruhusu matumizi yake kutoka Mamlaka ya Mawasiliano.

3.0 KUSIKILIZA SHAURI

Katika kusikiliza shauri la utetezi wa RIFARO AFRICA LIMITED:

1. Walikubali kupewa kibali cha kutumia rasilimali namba maalumu 15420 na kukubali pia kuwa matumizi yake yaliisha muda wake mwezi Julai, 2015;
2. Aidha walikubali kuwa Cheti Cha Matumizi ya Rasilimali Namba Maalumu 15420 kilipokwisha muda wake hawakuomba kuongezewa muda wa matumizi yake;
3. Hali kadhalika walikiri wameingia mkataba wa kibiashara na Kampuni ya Zanzibar Telecom Limited (ZANTEL) kwa ajili ya huduma ya Ezzy Pesa kama mtoa huduma mkubwa wa kampuni hiyo (mobile money super dealership).

4.0 MAAMUZI YA MAMLAKA

RIFARO AFRICA LIMITED imekuwa ikitumia rasilimali namba maalumu (VAS SMS CODE) 15420 bila cheti cha Mamlaka kuwaruhusu kufanya hivyo kinyume na Kanuni ya 17 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 (Electronic Communication Numbering and Addressing) Regulations, 2011.

Baada ya kutafakari utetezi wa Kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED na matokeo ya utetezo wao, Mamlaka inatoa maamuzi kama ifuatavyo:

1. RIFARO AFRICA LIMITED kulipa kwa Mamlaka faini ya shilingi milioni 10 (TZS 10,000,000) kwa kutumia rasilimali namba maalumu 15420 bila cheti cha kuruhusu kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano; na

2. RIFARO AFRICA LIMITED iache mara moja kutumia rasilimali namba maalumu 15420 kwa kuwa haina ruhusa ya kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuarifu umma kuwa RIFARO AFRICA Limited haina leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Kampuni hii ilikuwa na Cheti cha matumizi ya rasilimali namba maalumu 15420 ambacho kiliisha muda wake tangu mwezi Julai 2015.

Dkt. Ally Y. Simba
MKURUGEZI MKUU

02/03/2016
 
duh sasa hapo mbona majanga kwa sisi tuliotoa chetu kwa kiingilio. ila sisi na hii michezo duh
 
Si waende wakawanyang'anye!!! wanakuja kulalamika kwetu ili iweje!
 
Rifaro imekaa kiutapeli tapeli sana...bila shaka hata hicho cheti wamepewa baada ya kutoa rushwa huko tcra
 
Ukiichunguza rifora kiundani utagundua haina tofauti sana na DECI michezo ni ile ile panda kidogo vuna kingi zimebadilika nyakati tu Asante TCCRA kwa kuliona hili jipu, akili kumkichwa lasivyo mtapigwa kama deci, zama za ujanja ujanja utapeli na wizi zimeisha rungu ameshikilia mzinza a.k.a. msukuma acheni janja janja fanyeni kazi halali tumewachoka.
 
watakua na undugu na power club na deci hawa
Umesema DEC vyema iache ilivyo muasis wa dec tz alikuwa anayo nia ya kuinua maisha ya watz serekal ikazma ndoto zake,ebu ikumbushe utawala uliopo kurudisha bilion zilozuiliwa kwa wenyewe maskin utojibiwa na utaishia kuambiwa unaleta fyokovyoko utashughulukiwa
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
ISO 9001:2008 CERTIFIED

TAARIFA KWA UMMA

KUTUMIKA RASILIMALI NAMBA MAALUMU 15420 NA KAMPUNI YA RIFARO BILA CHETI CHA MATUMIZI YA NAMBA CHA MAMLAKA YA MAWASILIANO

1.0 UTANGULIZI

1.1. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni taasisi ya Serikali yenye jukumu la kusimamia huduma za Sekta ya Mawasiliano na Utangazaji nchini, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa rasilimali namba kwa mawasiliano na anwani kuhakikisha matumizi sahihi.

1.2. Katika siku za hivi karibuni, Mamlaka imeona taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu Kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano. Yafuatayo ni maelezo ya Mamlaka kuhusu taarifa hizo:

1.3.Mnamo tarehe 28 Julai, 2014 Mamlaka ilitoa kwa RIFARO AFRICA LIMITED Cheti cha Matumizi ya Rasilimali Masafa kwa ajili ya huduma za ziada za Mawasiliano kupitia SMS (VAS SMS CODE) namba maalumu 15420 kutumika katika kutengeneza mfumo wa Mawasiliano wa SMS kuunganisha na kupokea taarifa za mawakala wao wa kuuza na kusambaza muda wa maongezi kupitia wavuti yao (website);

1.4.Mnamo tarehe 27 Julai, 2015 Cheti hicho kilimalizika muda wake na Kampuni ya RIFARO Africa Limited haikuomba kuongeza muda wa matumizi wa rasilimali namba maalumu 15420. Kuendelea kutumia rasilimali namba hiyo bila cheti cha kuruhusu kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano ni ukiukwaji wa Kanuni ya 17 (1) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 - Matumizi ya Namba na Anwani za Mawasiliano - (Electronic Communication Numbering and Addressing) Regulations, 2011.

2.0 AMRI YA UTEKELEZAJI

Mnamo tarehe 24th Februari, 2016, Mamlaka ilitoa Amri ya Utekelezaji kwa kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED kwa mujibu wa Kifungu cha 45 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania sura ya 172 kama ilivyorekebishwa na Kifungu cha 179 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta, na kuimauru kampuni hiyo kufika mbele ya Mamlaka ya Mawasiliano kujitetea kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kuvunja na kukiuka Kanuni namba 17 (1) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2011 - Matumizi ya Namba na Anwani za Mawasiliano kwa kutumia rasilimali namba maalumu 15420 bila Cheti cha kuruhusu matumizi yake kutoka Mamlaka ya Mawasiliano.

3.0 KUSIKILIZA SHAURI

Katika kusikiliza shauri la utetezi wa RIFARO AFRICA LIMITED:

1. Walikubali kupewa kibali cha kutumia rasilimali namba maalumu 15420 na kukubali pia kuwa matumizi yake yaliisha muda wake mwezi Julai, 2015;
2. Aidha walikubali kuwa Cheti Cha Matumizi ya Rasilimali Namba Maalumu 15420 kilipokwisha muda wake hawakuomba kuongezewa muda wa matumizi yake;
3. Hali kadhalika walikiri wameingia mkataba wa kibiashara na Kampuni ya Zanzibar Telecom Limited (ZANTEL) kwa ajili ya huduma ya Ezzy Pesa kama mtoa huduma mkubwa wa kampuni hiyo (mobile money super dealership).

4.0 MAAMUZI YA MAMLAKA

RIFARO AFRICA LIMITED imekuwa ikitumia rasilimali namba maalumu (VAS SMS CODE) 15420 bila cheti cha Mamlaka kuwaruhusu kufanya hivyo kinyume na Kanuni ya 17 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 (Electronic Communication Numbering and Addressing) Regulations, 2011.

Baada ya kutafakari utetezi wa Kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED na matokeo ya utetezo wao, Mamlaka inatoa maamuzi kama ifuatavyo:

1. RIFARO AFRICA LIMITED kulipa kwa Mamlaka faini ya shilingi milioni 10 (TZS 10,000,000) kwa kutumia rasilimali namba maalumu 15420 bila cheti cha kuruhusu kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano; na

2. RIFARO AFRICA LIMITED iache mara moja kutumia rasilimali namba maalumu 15420 kwa kuwa haina ruhusa ya kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuarifu umma kuwa RIFARO AFRICA Limited haina leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Kampuni hii ilikuwa na Cheti cha matumizi ya rasilimali namba maalumu 15420 ambacho kiliisha muda wake tangu mwezi Julai 2015.

Dkt. Ally Y. Simba
MKURUGEZI MKUU

02/03/2016
Wakuu nimeona nichangie hili chapisho, huyu mtaalam kazichambua vizuri sana hizi sheria kuonyesha kuwa anaweledi wa kina, tatizo langu hiyo mitandao ya jamii ndio imemstua bila hiyo mitandao wasinge jua, je, hili lipo sawa kweli? Wito wangu nikuwaasa wafanye kazi kwa maslahi ya wananchi na sio maslahi yao binafsi, maneno mengiii porojo tupu fyuuuu. Nawasilisha.
 
SULUHISHO LA UVUMI WA KUFUNGIWA RFA!!!!!!!!
tunapenda kuwafahamisha kuwa taarifa zilizopo juu ya kufungwa kwa RFA sio sahihi

IKO HIVI mwanzon wakati RFA inatumia kampuni ya zantel ilikuwa inatumia code ya 15420 kwa ajili ya operations zote mf. Kuangalia timu ya watu ulionao. Sasa baada ya kuanza kutumia tovuti ya RFA yaan www.rifaroafrica.com na kuwa na Rifaro app wakaacha kutumia hiyo code(15420) hivo wakaacha hata kuilipia kama walivyokuwa wanafanya kabla.

Sasa TCRA ikaamua kuifungia hiyo code kwa sababu haitumiki tena na hailipiwi na RFA.kwa hiyo mfumo upo kama kawaida na kaz n mbele kwa mbele.na uvumi unaopostiwa na watu na network marketing zingne muupuzie ninyi fanyen kaz.MUELIMISHE NA MWINGINE...

Clous wametengua kauli hyo wagavi tu naendelea kupata malipo ya week jana
 
Kuna jamaa humu JF kuna threads kibaoooo ailikuwa anawavuta watu wajiunge wakatapeliwe,inaonekana alijua kwamba kufungwa kunakuja.

JF kuna matapeli kibaoooo,na ID zao zinajulikana sasa
Kuna yule Muuza viwanja kwa kupitia Bayport
Na kuna huyu mpiga debe wa RIFARO yumo humu pia
 
Back
Top Bottom