Kampuni ya MURO yatangaza kuuza mabasi yake, nini kipo nyuma ya pazia?

Awali ya yote tungeambiwa pia jinsi alivyopata hizo mali.

Kama kuna sintofahamu basi ni mfumo tu wa kawaida utakaomkumba kila aliyepata mali kwa mlango wa nyuma...huku kwetu tunaita 'karma'

Kama ulivuna pesa iliyomkosesha Mnyonge chakula au matibabu au maji masafi n.k. na ukadhani utaishi kwenye pepo yako milele basi you are wrong my friend.
acha chuki zako yeye atabaki kuwa tajiri tu kwa taarifa yako watakaoisoma namba ni watu wa chini kama wewe. ila punguza wivu wa kijinga
 
Swali la kujiuliza inakuaje yeye ameshindwa ili hali wengine wanazidi kutanuka? Kushindwa kwa kampuni kuna sababu nyingi tu tunaweza singizia mdororo wa uchumi kumbe njia za kifisadi za mwenye kampuni zimebanwa. Hizi biashara zina siri kubwa sana nyuma yake. Yeye anakaa pembeni wenzie wanazidi kutoa mabasi mapya kama kawaida. Vituo vingi vya mafuta vilivyojazana kuanzia kibaha mpaka Mlandizi vingi kazi yao kubwa ilikua ni kuchakachua mafuta ya Transit, yale hayana kodi yalikua yanashushwa pale then yanarudi jijini yanauzwa kwa bei ya kawaida sawa na yaliyolipiwa kodi. Sitashangaa nikianza kuona zile sheli zikifungwa moja baada ya nyingine kwa awamu hii
 
Mtikisiko wa Uchumi unaoendelea kutikisa kila mahali unadaiwa kusababisha Mmiliki wa Muro Investment kupiga bei mabasi 18.
 

Attachments

  • FB_IMG_1480272874950.jpg
    FB_IMG_1480272874950.jpg
    14.4 KB · Views: 55
Aisee, lets travel together!! Hii pamba ya zhong tong dsm to mwanza niliipenda sana
 
Sio kuyumba Kwa uchumi Mbona wengine ndo uzidi kuongeza mabasi mapya dabodabo siri anayo muuzaji
 
Wanaouziwa ni watanzania au wawekezaji kutoka nje na Ukiwa na watanzania watafanyia BIASHARA Tanzania au thinking aloud
 
Wanunuzi wanatoka wapi au uchumi umedorora kwake tu tukumbuke Mali ya dhulma uisha Pasi na faida Tanzania ya viwanda inakuja my foot
 
acha chuki zako yeye atabaki kuwa tajiri tu kwa taarifa yako watakaoisoma namba ni watu wa chini kama wewe. ila punguza wivu wa kijinga
Hiyo ni tafsiri yako ila pointi yangu ni hiyo hiyo...ukipata mali kimagumashi itarudi tu ilipotoka siku moja hata kama Mzee Magu hangekuwa raisi wa nchi.

Na wala simlengi Muro, la hasha...kama alipata mali yake kwa njia nyoofu kama vile kupitia kilimo n.k basi wala sie ninayemzungumzia hapa.....ila kama ulimvizia Mtu anayetoka Benki alafu umpige risasi umpore haki yake alafu utegemee utakula maisha raha mustarehe milele, la....kuna siku vitarudi vilipotoka.
 
Back
Top Bottom