Kampuni ya Jamii Media inahitaji "Office Attendant" nafasi moja (1)


Jamii Jobs

Jamii Jobs

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Messages
229
Likes
91
Points
45
Jamii Jobs

Jamii Jobs

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2014
229 91 45
Kampuni ya Jamii Media inahitaji mhudumu wa ofisi ambaye ataweza kusimamia na kufanya kazi zake za kila siku.

Majukumu ya mwombaji

Awe na uwezo wa kusimamia shughuli za kila siku za Kiofisi. Shughuli hizo ni Kufanya usafi wa ofisini, kufuatilia, kusimamia na kurekodi masuala ya chakula cha timu yote ya Jamii Media, Kununua na kusimamia mahitaji ya jikoni, kushiriki na kuhudumia katika Matukio yanayohusiana na Jamii Media, kujifunza majukumu na kuyatambua pamoja na uwezo wa kujisogeza katika majukumu.

Sifa za Mwombaji

Awe ni Mwanamke
Awe na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea
Awe anajua kusoma na kuandika
Awe mkazi wa Dar es Salaam
Awe tayari kufanya kazi kwa mabadiliko na si kwa mazoea

Muda Wa Kazi


Jumatatu – Ijumaa: Saa 2 Asb mpk Saa 11 Jioni
Jumamosi na siku za Sikukuu: Saa 2 Asb hadi Saa 7 Mchana
Jinsi ya kutuma Maombi

Unaweza kutuma maombi kwa njia mbili tofauti

1. Tuma barua pepe (email) kwenda vacancies@jamiiforums.com ikiwa na kichwa cha habari “Office Attendant”, kisha eleza ni kwa nini tukuchague wewe kwa nafasi hiyo.

AU

2. Tuma ujumbe wa whatsapp kwenda namba 0745 200 717 (TAFADHALI USIPIGE), anza ujumbe wako kwa kichwa cha habari “Office Attendant”, kisha eleza ni kwa nini tukuchague wewe kwa nafasi hiyo. Hakikisha ujumbe huo unauandika kwa pamoja na usiutenganishe.

Mwisho wa kuomba 22, Julai 2016
 
M

Mtafuta kiki

Member
Joined
Jun 3, 2016
Messages
76
Likes
32
Points
25
Age
48
M

Mtafuta kiki

Member
Joined Jun 3, 2016
76 32 25
Nmetuma kwny namba ya whatsapp ila naona kama haitumiki! Mtoe feedback kama mmepata
 

Forum statistics

Threads 1,236,696
Members 475,218
Posts 29,266,972