Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
ZAIDI ya kampuni 500 kutoka Ulaya, Marekani na Asia zinapigana vikumbo kuwania mikataba mbalimbali ya tafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi barani Afrika, FikraPevu inaripoti.
Uchunguzi unaonyesha kwamba, kuwepo na kugundulika kwa akiba kubwa ya mafuta na gesi barani humo kumevutia uwekezaji wa moja kwa moja (Foreign Direct Investment) kutoka Marekani, China na nchi nyingi za barani Ulaya.
Rasilimali za mafuta na gesi, zikichangiwa na rasilimali nyingine kama madini, zilimelifanya Bara la Afrika kuwa kipaumbele katika uwekezaji kwa mataifa hayo, ambapo kampuni zao – nyingi zikisaidiwa na serikali za nchi zinakotoka – zimefanikiwa kupata mikataba minono ya kufanya tafiti na kuchimba mafuta na gesi, nishati ambazo zina soko la uhakika licha ya kuporomoka kwa bei ya mafuta kwa kipindi hiki.
ZAIDI...