Losambo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 2,611
- 867
Ni wengi hawajui kuwa kampeni zinazoendelea hivi sasa hazina madhara sana kwa wapiga kura kwa sababu wengi walishajua ni mgombea yupi watayempigia kura. CCM inajidanganya sana kwamba mgombea wao Magufuli anakubalika lakini wanasahau matendo ya CCM yameshahubiri miaka 10 ya Kikwete zaidi anachohubiri Magufuli jukwaani! Hebu jiulizeni, kama mgombea wa urais anasema atamaliza tatizo la mgao wa umeme ambalo limedumu kwa takribani 30yrs bila suluhu ya maana!! Ni mkoa gani ambao hauna mgao wa umeme saizi???
Hebu jiulize Magufuli anasema ataboresha makazi ya walimu ambao hata madei yao serikali inawapiga danadana! Embu jiulize kama serikali inashindwa kutekeleza bajeti yake katika wizara nyeti kutokana na ukata, unafikiri uhodari wa Magufuli unaweza kuwabadilisha nini watu waliochoka na hadaa hizi??
Hebu jiulize machinga, watu wa bodaboda watahuburiwa nini ili mioyo yao iwe safi na kumpa kura Magufuli wakati kila siku wananyanyaswa na serikali hiyo hiyo??? Hebu jiulize mkulima aliyecheleweshewa pembejeo zake, akalanguliwa kisha akaishia kukopwa na serikali na hajui atalipwa lini atahuburiwa nini Magufuli aelewe??
Hebu jiulize watu ni watu wangapi waamini jembe Magufuli atafufua viwanda kweli kama siyo hadaa ili apate kura tu??? Tatizo ni mfumo wa CCM ambao umewafanya wananchi wawe wamepiga kura kabla ya tarehe 25 - Oct isipokuwa ni wachache wanajua hilo.
Kuja kwa Lowasa ni kama zali tu kwa UKAWA, lakini ukweli waliobaki CCM wataendelea kubaki huko na waliopo UKAWA wataendelea kubaki.
Na ndiyo maana nasema kampeni zimekwisha ila watu hawajui tu. RAIS atatoka upande ule ambao una mashabiki wengi saizi mjini na vijijini angalau 55%.
NAHITIMISHA Raisi wananchi wanamjua tayari, kampeni ni suala utaratibu ila hakuna ambaye atahadaika na mchakato huo.
MATENDO YA SERIKALI HUUBIRI ZAIDI KULIKO LONGO LONGO ZA MAJUKWANI.
NAWASILISHA.