Kampeni za uraisi

Kampeni za uraisi

Crook

Senior Member
Joined
May 8, 2015
Posts
137
Reaction score
110
Kwakuwa kampeni za uraisi zinaanza leo basi moja kwa moja tiririsha sera za wagombea wako kutoka maeneo mbali mbali KARIBUNI!
 
Mbili kubwa:

1. elimu bora na sio bora elimu

2. kukuza uchumi hadi wakenya na warwanda watutafute kwa tochi
 
Zimekuwepo sababu kadhaa ambazo watu kadhaa wamejaribu
kuziweka hapa wakionyesha ndio chanzo cha watu kufurika
kuhudhuria uwepo wa Lowassa mahali fulani baada ya kutangaza
kujiunga na UKAWA/CHADEMA.
Ni kuwa kabla palikuwepo na kukata tamaa kwa kiwango kikubwa
kwa Watanzania kuelekea ndoto yao ya kuiondoa ccm katika
kutawala. Watanzania waliivumilia ccm kuwa inaweza kufanya
mabadiliko yake ya ndani ambayo yangeweza kuleta maisha bora
kwa Watanzania. Kusubiri kwa mabadiliko haya kumekuwa siku
zote hakufanyiki na sana sana kinachofanyika ni kuimarisha
mfumo ambao muda mrefu sana Watanzania waliisha ukinai. Mtu
anazaliwa katika mfumo huo unao mpatia umaskini hadi anazeeka
katika huo mfumo.Watanzania walifika mahali wakajiimanisha
kuwa sio rahisi kuiondoa ccm katika utaratibu huu wa kupiga kura.
Katika utaratibu huu wa amri na kanuni za Demokrasia za ccm
ambazo zimekaa kisanii. Kujua kuwa waliisha kata tamaa
Watanzania wengi wamekuwa hawaoni sababu hata ya kwenda
kupiga kura kwa muda mrefu sasa. Mfano ni mwaka 2010, walio
piga kura ni chini ya nusu ya waliokuwa wamejiandikisha.
Watanzania ni wapenda amani. Amani ya Watanzania ilikuwepo
hata kabla ya Uhuru. Mkoloni aliwakuta Watanganyika wakiwa na
amani kiasi cha kuwatia bakora huku wakiwa kimya. Hivyo
Watanganyika/Watanzania wanahitaji fulsa ili wafanye mabadiliko
ya amani na si rahisi wakalazimisha mabadiliko kwa kutumia
siraha hata uwe umewaonea kwa kiasi gani.
Mwaka 1995 wakati Mrema alipojitokeza Watanzania waliona ni
fulsa ya pekee ya kuiondoa ccm. Kwa namna ccm ilivyofanya
hakuna anayeelewa kilichitokea na kila mmoja alibaki na sababu
zake. Hata mwaka 2010 mambo yalikuwa hivyo hivyo.
Sasa ni kuwa ametokea Lowassa. Watanzania wanaona hii ni fulsa
nyingine ya kutimiza ndoto zao.
Kinacho waaminisha kuwa ndoto yao sasa inaenda kutimia ni:
1. Nyerere alisema atakaye yaleta mabadiliko ambayo Watanzania
watakuwa wanayataka atatoka ccm.
2. Watanzania wanaamini Lowassa atakuwa anajua siri ambazo
ccm huwa wanatumia kuvuka kizingiti cha kukataliwa na wapiga
kura lakini bado ikaonekana wameshinda. Watanzania wana imani
kuwa iko siri ya ushindi tofauti na kura zinazopigwa
3. Watanzania wengine hudhani huwa kuna kuzidiwa kifedha kitu
ambacho Wapinzani huwa hawana sasa wanatumaini hili Lowassa
atalitatua maana nyuma ameonyesha kuweza ktk harambee
kadhaa.
4. Mikakakati mingi ya kushinda aliyo nayo Lowassa.
Sasa ukichanganya na kiwango ambacho Cdm wamefikia, kiwango
ambacho CDM ilihamasisha watu kujiandikisha, Watanzania
wamepata shauku ya kuyaona mabadiliko.
Ndani ya shauku hii Watanzania huwezi kuwambia chochote.
Hakuna propaganda itakayobadili mwelekeo. Sasa mafuriko
hayajaonekana subiri Kampaini zianze.
Natabiri mwaka huu pia kutakuwepo na mafuriko ya wapiga kura
kujitokeza kwenye kupiga kura.
 
Jama watanzania wazalendo mlioko nyumbani mpige kampeni ya nguvu, ccm iondoke madarakani, angalau nchi iPate mabadiliko kutoka ukawa..zifnyike reform mbali mbali kwenye sekta ya afya, elimu, mahakama, uchukuzi, miundombinu nk..jama kampeni ya mtu mmoja mmoja na viongozi ukawa wajitahidi kuzuia mianya ya kuibiwa kwa uchaguzi..hiki ndo kipindi chenyewe
 
Kutunza na kuwatibu tembo watakao jeruhiwa kwa bahati mbaya.
 
Back
Top Bottom