Kampeni Za Uchaguzi: Nasubiria

Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
458
170
Kampeni za manyanga, nesema zinanikera
Wenyewe munazipanga, nasisi tunawachora!
Mfano wenu wajinga, mwaonekana uchwara!
Nasema munanikera, kwa vyenu vyote vimbwenga!


Nasubiria novemba, ambapo zitapotea
Mujitangaze umwamba, na suti kujivalia
Kwa sasa mwaficha pamba, suti zenu asilia
Najua zitapotea, batiki na vyo vilemba


Kwa sasa zimefichika, nizisemazo ni suti
Na nyote mwacheka cheka, mwaogopa kula buti
Vigoda pia mikeka, mwakalia hati hati
Imeshakuwa shuruti, kila kona mwaoneka!


Novemba twasubiria, mje ingia mitini
Muanze kutukimbia, kujificha ofisini
Ni kura mwapalilia, ujanja wakizamani
Utadhaninia watani, kwa kura mkililia


Nasema mushatuchosha, twawajua miyeyusho
Kwa dhati ninawapasha, wengi wenu ni michosho
Uthadhani washawasha, wakati mwataka posho
Roho zenu za korosho, na mimi nawajuslisha!



 
Back
Top Bottom