kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 256
Nimefuatilia mikutano ya kampeni za uchaguzi na kugundua kwamba pamoja na ilani zinazotangazwa na vyama ambazo ndio dira ya yajayo, lakini kikubwa na kinachotofautishwa na vyama hivi ni kauli za ''TUMEFANYA'' na ''TUTAFANYA''
Kwa wale wenye kuelewa kati ya hizi kauli mbili moja ni rahisi kuikubali kwa sababu unaweza kuwa umeona hicho kinachosemwa tumefanya ni rahisi kukubali na kuunga mkono kwa kuwa uthibitisho upo.
Hii kauli ya pili tutafanya ina mambo mengi na tutangulize Mungu akipenda kwani lolote laweza kutokea ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, mabadiliko hali ya uchumi wa Dunia na siasa za mataifa mengine.
Kwa maelezo hayo hapo juu Ndugu John Magufuli anastahili kupewa hii nafasi ya kuwa Rais, amefanya mengi kupitia uongozi wake, wasaidizi wake na Serikali yake kwa ujumla.
Hakuna asiyeyaona, wala asiyeyasikia na kuthibitisha kila kona ya nchi hii ndani ya miaka mitano tu kuna alama za maendeleo zimebaki na zitaendelea kubaki kwa manufaa ya nchi hii.
Kuna usemi mmoja unasema ''safari moja huanzisha nyingine'', Safari hii ndugu zangu wenye akili na ufahamu kwa Magufuli tena aendeleze safari nyingine za maendeleo Tanzania itakuwa gumzo kwa vizazi vijavyo!!