Kamjadala kwenye daladala leo

Mabagala

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,477
325
Nimejichokea zangu narudi kutoka kazini, niko kwenye usafiri wetu wa jumuia. Foleni ilipoanza kunoga basi kamjadala kakaanza mara baada ya kupita kibasi kikiwa na abiria wenye nguo za njano na kijani (sikuelewa ni wana yanga ama wana Chama Cha Matamu). Kama utani vile mjadala ukaanza. Jamaa kadai maisha magumu kwa upande wake yamesababishwa na mama yake. Kama mama yake angekuwa mjanja basi angemdate fisadi mmoja wapo na yeye asingezaliwa katika familia duni! Hoja mbali mbali zilitolewa hadi uchovu wa foleni ukasahaulika. Nilisahau uchovu wa foleni pale jamaa alipodai viongozi wanadai wameongeza ajira kwa kuangalia vijana waokotao vyuma chakavu na machupa ya maji yaliyokwisha tumika. Nimejikuta nimeshafika safari yangu, sijui huko mbele mjadala umeishaje! Ila nina hakika mijadala ya kwenye usafiri wa daladala huwa haina hitimisho. Wale mlio na usafiri binafsi mnakosa mijadala kama hii!

Mungu irehemu nchi yetu
 
Yaani mama yake angekuwa kiburudisho cha zuzumagic Roast Hamu?
Kudadadeki, ana laana huyu kwa kumuuza mama yake kwa VIPANDE VYA FEDHA
 
Hahahahahaa..........ni kweli,hata hivyo wale wanaopanda treni ndio wanafaidi mengi
 
Kwa daladala zina raha yake wajameni sio siri shida ni hiyo kubanwa na kukanyagwa na kuchafuliwa nguo zako hiyo tu ndo mie sipendi
 
We huoni kila sehemu ni malalamiko tu hata kwa watoto wadogo!
 
Kwa daladala zina raha yake wajameni sio siri shida ni hiyo kubanwa na kukanyagwa na kuchafuliwa nguo zako hiyo tu ndo mie sipendi

Hapo kwa kukanyagana na kusukumana ndio issue. Ila kama umepata siti mbona burudani
 
Kwatreni si unajua mwendo mrefu. hAPO Ubahatike kusafiri DAR mpaka Mwanza ama kigoma ndio utafaidi mijadalla vizuri. Ila sina uhakika kama viti bado ni vya chuma ama bati. labda siku izi wameboresha

Hahahahahaa..........ni kweli,hata hivyo wale wanaopanda treni ndio wanafaidi mengi
 
Bujibuji ndivyo jamaa alivyoanza kwa kuelekeza lawama kwa mama yakekwamba kwanini haukujilengesha kwa fisadi, yeye kamfata maskini (baba yake) ndio maana maisha yake yanakuwa ya tabu sasa!
Yaani mama yake angekuwa kiburudisho cha zuzumagic Roast Hamu?
Kudadadeki, ana laana huyu kwa kumuuza mama yake kwa VIPANDE VYA FEDHA
 
Dala dala raha sana, ishu inakuja kwenye kubanwa na kuibiwa. Makonda huwa wananipa raha sana na misemo yao.
 
Juzi nilimsikia dokta mwinyi kasema hata mtu hai unaweza kumwita marehemu coz kila mtu anahitaji rehema za mwenye mungu
 
Back
Top Bottom