Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Simon Siro Kamishna wa Jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam leo tarehe 17.05.2016 ameongea na Waandishi wa Habari na kutanabaisha kuwa Jeshi la Polisi limewakamata vijana waliokuwa wakifanya vitendo vya kihalifu katika viunga mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam maarufu kama Panya Road wanaofikia 75. Vijana hao wamekamatwa wakiwa na Mbwa na Jeshi la Polisi limekamata na Mbwa hao pia. Kamishna Simon Siro akaongeza kuwa hao mbwa wamesumbua sana maeneo ya Mbade
Aidha Kamishna Simon Siro akitoa pia taarifa ya kuwa mnamo tarehe 27.04.2016 saa 3:30 asubuhi silaha (Bunduki) aina ya Short Gun yenye nambari 7264 iliyokatwa mtutu ilikamatwa huko Mbagala Chamazi lakini haikuwa na risasi. Silaha hiyo ilikamatwa baada ya raia wema kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.
Kamishna Simon Siro akaongeza pia kuwa zoezi la uhakiki wa silaha linaendelea hivyo watanzania wanaombwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na vyombo vya usalama.