Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova Aagwa, Aomba kazi Tena Polisi

vantz

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
1,107
570
d55a551723cbde7d73dd5c7a54be01c1.jpg


Aliyekuwa kamanda wa kanda maalumu ya Dar es laam, Suleiman Kova, akiagwa muda huu katika viwanja vya chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Uaskari Moshi (MPA) Zamani kikijulikana kwa jina la CCP

========

Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova Aagwa...... Aomba kazi Tena Polisi
1.jpg

Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, ameliomba jeshi hilo kumpa kitengo cha masoko ili aweze kulitangaza na kuliunganisha na wananchi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maboresho ndani ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.

Kova alitoa ombi hilo jana mjini Moshi katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Shule ya Polisi Moshi (MPA).

Alisema jeshi hilo linaelekea kuzindua mpango wake wa matokeo makubwa sasa (BRN) ,ambao unahitaji msukumo wa jamii katika kusaidia kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali ukiwamo wa mtandaoni na dawa ya kulevya.

Kova alisema kutokana na utumishi wake wa zaidi ya miaka 40 kwa kushirikiana na wastaafu wengine, wanaweza kusaidia na kuwa kiunganishi baina ya polisi na raia kama njia bora ya kukabiliana na uhalifu kwa kutumia kitengo cha masoko.

“Nimekuwa mtumishi ndani ya polisi kwa miaka 40, ninaweza kutumika hata na Shule ya Polisi Moshi kufundisha na hata kutoa uzoefu wangu ambao utalisaidia jeshi katika kukabili uhalifu, kama mnavyoniona ninazo nguvu za kutosha na ninalipenda Jeshi la Polisi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kova aliiomba serikali kuliboresha zaidi jeshi la polisi kwa vifaa, mbinu na teknolojia za hali ya juu ili kukabiliana na matukio ya uhalifu wa aina mbalimbali unaokuwa kulingana na ukuaji wa teknolojia duniani.
2.jpg

3.jpg

4.jpg
Chanzo: Mpekuzihttps://4.bp.blogspot.com/-mrdskjpW...AoTUENMMyxaTo6msrClidCHuBmFXQCLcB/s1600/4.jpg
 
Karibu sana uraiani uwenda ukajifunza kitu kizuri sana nje ya jeshi, hasa swala la kupiga watu mabomu ya machozi pasipo sababu za msingi. Nahisi unaweza kuwa mtetezi mzuri kwa hilo, manna ikitokea yakapigwa tunakimbilia kwako vijana wanapiga uko uko na wewe unapata hali halisi utakayotetea kama raia mwenzetu.
Karibu sana X Commandant.
 
Hicho kichwa kimenishtua sana, nilijua kuna habari yake imenipitia pembeni.
 
Karibu sana uraiani uwenda ukajifunza kitu kizuri sana nje ya jeshi, hasa swala la kupiga watu mabomu ya machozi pasipo sababu za msingi. Nahisi unaweza kuwa mtetezi mzuri kwa hilo, manna ikitokea yakapigwa tunakimbilia kwako vijana wanapiga uko uko na wewe unapata hali halisi utakayotetea kama raia mwenzetu.
Karibu sana X Commandant.
Usijidanganye huyu anaenda kuchukua fadhila zake kama si kupewa ukuu wa mkoa basi ataanza na wilaya.
 
Aaaaaahhh kumbe, mi nilipoona kichwa cha habari nikajua anaagwa kila mkoa na polisi, kumbe kaenda kuagwa chuoni
 
Back
Top Bottom