Kamera 10 zafungwa daraja la Mfugale

Kamera 10 zafungwa daraja la Mfugale

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
1095194

KAMERA 10 kati ya 16 zinazotakiwa kufungwa kwenye Daraja la Juu la Mfugale eneo la Tazara jijini Dar es Salaam, zimeshafungwa hadi sasa. Kamera sita zilizobaki, zitafungwa wakati wowote, baada ya nguzo kubwa inayosubiriwa kuletwa.

Akizungumzia na gazeti hili kwa simu, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Mikataba cha Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam, Abednego Lyanga alisema kazi hiyo, ilitakiwa iwe imekamilika mwishoni mwa mwezi uliopita. Lyanga alisema hata hivyo mkandarasi, Kampuni ya E 1, alishindwa kutokana na sababu za msingi ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa nguzo kubwa alizoagiza nje ya nchi kuka, zinazotumika kufunga kamera.

“Hadi sasa kamera 10 zimeshafungwa, mbili zilifungwa mwishoni mwa Januari mwaka huu na kamera nyingine nane zimefungwa siku chache zilizopita na zilizobakia zipo ila kilichokuwa kinasubiriwa ni nguzo kubwa zilizoagizwa nje ya nchi,” alisema Lyanga.

Alisema mkandarasi aliongezewa muda na mwezi huu atakabidhi kazi, baada ya kufunga kamera hizo na kufanya majaribio. Alisema katika daraja hilo na eneo hilo kwa ujumla, zinahitajika kamera 16 zitakazokuwa zikionesha matukio yote yanayoendelea hapo, na iwapo makosa ya usalama barabarani yatafanywa na madereva, itakuwa rahisi kuwabaini na kuchukua hatua.

Lyanga alisema kamera 10 zilizofungwa, zinaendelea kufanya kazi sasa na zinaonesha matukio yote yanayoendelea darajani na zitaendelea kufanya kazi muda wote. Lengo la kuziweka ni kuhakikisha miundombinu ya eneo hilo, inakuwa salama, na kuwabaini madereva wanaokiuka sheria za barabarani ili vyombo husika viwachukue hatua.

Agizo la kufungwa kamera hizo lilitolewa Septemba 27, 2018 na Rais John Magufuli wakati akizindua daraja hilo. Rais alisitiza kuwa kamera hizo, zitawabaini wananchi wanaoendesha vyombo vya moto bila kufuata taratibu, wakiwemo madereva walevi.

Miezi mitatu baada ya agizo hilo la Rais Magufuli, utekelezaji ulianza kwa kamera mbili kufungwa mwishoni mwa Januari mwaka huu, kisha tena kamera nane zimefungwa hivi karibuni. Kinachosubiriwa ni nguzo kufungwa ili kamera sita zilizobaki zifungwe.

Lyanga alisema gharama za uwekaji kamera hizo zote, umegharimu zaidi ya Sh milioni 100. Alisema kamera hizo zinaonekana mubashara na wanaweza kuangalia mwenendo mzima wa watumiaji daraja hilo. Daraja hilo lina urefu wa meta 425 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa meta 287 kila upande, na hivyo kufanya daraja lote kuwa na urefu wa kilometa moja. Ujenzi wake uligharimu Sh bilioni 106.9.
 
Chadema watanuna mno kwa ahadi hii kutekelezwa
 
Usije ukatamka serikali ndiyo imetoa pesa. Fedha za ujenzi wa daraja lile zilikuwa za msaada wa walipa kodi wa Japani (kaangalie "site board " usome ili ujuwe Jiwe anavyowahadaa watu). Jiwe aende nje akatafute misaada kwa hao anaowaita mabeberu bila hivyo kila kitu kitamshinda kama ujenzi wa barabara ya kimara - chalinze
 
Limbukeni kwa kukurupuka na kutoa maagizo hats ambayo hayakuwepo kwenye plan .Badala ahangaike kutekeleza ilani ya chama chake laptop na milioni hamsini kila kijiji ,yeye anahangaika na kutafuta sifa .
 
Kugunga kamera 10 sasa ukizia thaman ya hiyo kandaras kama hujaambiwa million 500!!!
 
View attachment 1095194

KAMERA 10 kati ya 16 zinazotakiwa kufungwa kwenye Daraja la Juu la Mfugale eneo la Tazara jijini Dar es Salaam, zimeshafungwa hadi sasa. Kamera sita zilizobaki, zitafungwa wakati wowote, baada ya nguzo kubwa inayosubiriwa kuletwa.

Akizungumzia na gazeti hili kwa simu, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Mikataba cha Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam, Abednego Lyanga alisema kazi hiyo, ilitakiwa iwe imekamilika mwishoni mwa mwezi uliopita. Lyanga alisema hata hivyo mkandarasi, Kampuni ya E 1, alishindwa kutokana na sababu za msingi ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa nguzo kubwa alizoagiza nje ya nchi kuka, zinazotumika kufunga kamera.

“Hadi sasa kamera 10 zimeshafungwa, mbili zilifungwa mwishoni mwa Januari mwaka huu na kamera nyingine nane zimefungwa siku chache zilizopita na zilizobakia zipo ila kilichokuwa kinasubiriwa ni nguzo kubwa zilizoagizwa nje ya nchi,” alisema Lyanga.

Alisema mkandarasi aliongezewa muda na mwezi huu atakabidhi kazi, baada ya kufunga kamera hizo na kufanya majaribio. Alisema katika daraja hilo na eneo hilo kwa ujumla, zinahitajika kamera 16 zitakazokuwa zikionesha matukio yote yanayoendelea hapo, na iwapo makosa ya usalama barabarani yatafanywa na madereva, itakuwa rahisi kuwabaini na kuchukua hatua.

Lyanga alisema kamera 10 zilizofungwa, zinaendelea kufanya kazi sasa na zinaonesha matukio yote yanayoendelea darajani na zitaendelea kufanya kazi muda wote. Lengo la kuziweka ni kuhakikisha miundombinu ya eneo hilo, inakuwa salama, na kuwabaini madereva wanaokiuka sheria za barabarani ili vyombo husika viwachukue hatua.

Agizo la kufungwa kamera hizo lilitolewa Septemba 27, 2018 na Rais John Magufuli wakati akizindua daraja hilo. Rais alisitiza kuwa kamera hizo, zitawabaini wananchi wanaoendesha vyombo vya moto bila kufuata taratibu, wakiwemo madereva walevi.

Miezi mitatu baada ya agizo hilo la Rais Magufuli, utekelezaji ulianza kwa kamera mbili kufungwa mwishoni mwa Januari mwaka huu, kisha tena kamera nane zimefungwa hivi karibuni. Kinachosubiriwa ni nguzo kufungwa ili kamera sita zilizobaki zifungwe.

Lyanga alisema gharama za uwekaji kamera hizo zote, umegharimu zaidi ya Sh milioni 100. Alisema kamera hizo zinaonekana mubashara na wanaweza kuangalia mwenendo mzima wa watumiaji daraja hilo. Daraja hilo lina urefu wa meta 425 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa meta 287 kila upande, na hivyo kufanya daraja lote kuwa na urefu wa kilometa moja. Ujenzi wake uligharimu Sh bilioni 106.9.
Zitazinduliwa lini na kifutu mkuu??
 
Polisi wanaochukuwa rushwa kwa madereva wa magari mlangoni mwa kiwanda cha Bakhresa baada ya kuvuka reli camera zinawaona?
 
Back
Top Bottom