Kamati ya Utendaji ya TFF yaketi leo

Kamati ya Utendaji ya TFF yaketi leo

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Leo jumapili tarehe 24, Mei 2015 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF imeketi katika ukumbi uliopo makao makuu ya Shirikisho uwanja wa Karume.

Kamati ya Utendaji imepitia masuala mbalimbali na kutoa maamuzi yafuatayo:

CLUB LICENCING (Leseni za vilabu) Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16.

KOMPYUTA - Kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.

MFUKO WA FDF - Kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, kikao cha Kamati ya Utendaji wa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.

Aidha kikao hicho kimeteua wajumbe wafuatao wawe wajumbe wa
tume hiyo
(i)Tido Mhando - Mwenyekiti,
(ii) Deogratius Lyatto - Makamu mwenyekiti
(iii)Ephraim Mafuru - mjumbe,
(iv)Beatrice Singano - mjumbe,
(v)Joseph Kahama - mjumbe
(vi)Ayoub Chamshana - mjumbe.

Pia Henry Tandau ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa mfuko huo.

AJIRA
Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini kuanzia tarehe 01, Juni 2015.

Wambura kabla ya uteuzi huo alikua mkurugenzi wa mashandano TFF.

TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu.

Kamati ya utendaji imemteau Martin Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashandano TFF.

TIMU ZA TAIFA
Kamati ya utendaji ya TFF imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya Cosafa.

Kikao cha kamati ya utendaji kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.

Baada ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.

Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi.

Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.

Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 - 2012.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
 
Malinzi pia umeshindwa sio kocha peke yake, nawe ujitasmin huja fanya lolote la maana mpaka sasa, zaid ya kuleta ile mijezi yako isiyokua na mvuto.
 
Asee upuuz at its climax powered by ujinga!! Yaani wampe muda avuruge na CHAN ndo wamtimue??
 
Football Admin wazuri ni Said el Maamry na Rage.huyu wa pili hafai ubunge lakini kwenye football anajuwa saana Lobbing za kimataifa
 
kwa Mukebezi, ni makosa makubwa, haiwezekani kila ajira, ya TFF, ni mpaka uwe muhaya. Hivi, makabila mengine, hayana, werevu?
 
Duh hawa Ndio viongozi wetu wanafikiri kwa kutumia masaburi
 
Hawa wamekula maharage ya wapi hawaaaa
 
Sipendi kabisa kuwa na fikra za ukabila...Lakini kwa hili la uteuzi wa Leopold Mukebezi....Napigia msitari
 
kwa Mukebezi, ni makosa makubwa, haiwezekani kila ajira, ya TFF, ni mpaka uwe muhaya. Hivi, makabila mengine, hayana, werevu?

Waliopo tayari ni wengi kwa vigezo vyovyote vile. Bado anaongeza wengine.

Wanampa muda zaidi Nooj lakini Kim Poulsen hakupewa muda huo.
 
Waliopo tayari ni wengi kwa vigezo vyovyote vile. Bado anaongeza wengine.

Wanampa muda zaidi Nooj lakini Kim Poulsen hakupewa muda huo.

katika maaamuzi ya kipumbavu zaidi kuwahi kufanywa ni ya Kumtimua Kim

Kwa mwendendo wa timu chini ya Kim tungekuwa mbali saana

Amekuja huyu mwehu mwingine amefanya nini kwenye mpira wetu

Na bado malinzi kwa wingi wa makamasi wanampa avurunde tena CHAN

Malinzi tokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa....hatukutakiiiiiiiiiiiii...wewe ndio tatizo kwenye mpira wetuu

Malinzi hufaiiiiii

Tokaaaaaaa

Kiongozi huna la maana ulilofanya hadi sasa,...uozo mtupu..sisi ni wa kufungwa na swaziland? kweli? kweli?

Malinzi sasa imetosha...It is high time utupishe...Bora arudi tenga aokoe jahazi

cc Jamal Malinzi Makoye Matale Amavubi sembo Bantu lady nifah
 
Last edited by a moderator:

Anampa muda maana hela ya fidia hana kwa sasa. Amefuja hela kwenye ofisi mjini na upuuzi wa maboresho ambayo matunda ndiyo vipigo vitatu cosafa.
 
Last edited by a moderator:
Football Admin wazuri ni Said el Maamry na Rage.huyu wa pili hafai ubunge lakini kwenye football anajuwa saana Lobbing za kimataifa

Kijana umezaliwa mwaka gani wewe?

Unamaanisha Rage katibu mkuu wa zamani wa FAT?
 
Timu yetu ya taifa kiukweli inakera mno...
 
jamaa ni mzigo sana, ina maana Tz hatuna kabisa mshambuliaji mwenye uchu wa kufunga magoli?

Wachezaji wazuri na wenye vipaji wapo wengi sana mikoani huko...

Kitu wanachokosa ni ushauri wa kiufundi na exposure ya mechi kubwa kubwa...

Lakini TFF na makocha wao kila mwaka wanatuwekea Bocco na wapuuzi wenzake...

Yaani siku ambayo Stars wanacheza bila Samatta au Ulimwengu wala huwa sihangaiki kufuatilia matokeo maana najua hatutashinda...
 
Back
Top Bottom