Kamati ya PAC: Cheyo na Zitto ngoma nzito

Kamati ya PAC: Cheyo na Zitto ngoma nzito

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
View attachment 86943

John-Cheyo.jpg

Posted Alhamisi,Marchi14 2013

Hatimaye Bunge limetangaza mabadiliko ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge zinazotarajiwa kuanza kukutana kuanzia Jumatatu ijayo, huku baadhi ya vigogo wakiwekwa katika kamati moja na kufanya zoezi la kuchagua wenyeviti wa kamati hizo kuwa gumu.

Uteuzi wa majina ya wajumbe hao unakuja mwezi mmoja tangu kumalizika kwa Mkutano wa 10 wa Bunge ambapo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitangaza mabadiliko ya kamati hizo, huku akiifuta Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. Kutokana na mabadiliko hayo, shughuli za POAC sasa zitafanywa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).

Kamati nyingine iliyofutwa ni ile ya Sheria Ndogo wakati zimeundwa kamati mpya za Bajeti, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na ya Ulinzi na Usalama. Majukumu ya Kamati ya Bajeti ni kufuatilia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali na sera za fedha pamoja na kuainisha na kupendekeza vyanzo vya mapato ya Serikali na kufuatilia mwenendo wa uchumi. Wajumbe waliokuwepo POAC ambao wamehamishiwa PAC ni Zitto Kabwe, Deo Filikunjombe, Ester Matiko, Zainab Kawawa na Kheri Ali Khamis.

Kamati ya PAC ni lazima iwe na mwenyekiti kutoka kambi ya upinzani, hali inayofanya uchaguzi wake kuwa mgumu kwa kuwa Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo naye ni mjumbe wa Kamati hiyo. Cheyo anatazamiwa kupata upinzani mkali kutetea kiti chake kwani atapata upinzani mkali kutoka kwa Zitto, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya POAC.

Kuna tetesi tayari kuwa Zitto, ambaye alilalamikia kitendo cha kuvunjwa kwa kamati ya POAC, ameanza kampeni za chinichini ili kumtoa Cheyo, ambaye ameshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2005. Wengine ambao walikuwa wajumbe wa POAC ambao wamehamishiwa Kamati ya Nishati na Madini ni Jerome Bwanausi na Murtaza Mangungu, pia katika kamati hiyo ya Nishati na Madini kuna wajumbe wapya ambao ni Anne Kilango na David Silinde.

Wengine waliokumbwa na mabadiliko hayo ni Grace Kiwelu ambaye amehamishwa kutoka Kamati ya Miundombinu kwenda Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira sambamba na John Mnyika na Ester Bulaya.

Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustino Mrema ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ametupwa katika kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, pia Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi akibaki katika kamati hiyo, pia yuko katika Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo imemegwa kutoka katika Kamati ya Mambo ya Nje ambayo hivi sasa inaitwa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati hiyo kabla ya kugawanywa, Edward Lowassa pamoja na makamu wake Mussa Azzan Zungu wamekuwa wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Katika uteuzi huo Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia, amekuwa mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge na Kamati ya Bajeti, huku Andrew Chenge, Tundu Lissu, Christopher Ole Sendeka pamoja na Zungu wakiwa katika Kamati ya Kanuni za Bunge. Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Iddi Azzan amepelekwa katika Kamati ya Masuala ya Ukimwi.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye awali alikuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi, sasa amekuwa mjumbe wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara ambayo imeunganishwa na kuwa moja.

Natumaini rushwa ya aina yoyote haitatumika ikizingatiwa itikadi za wagombea ni tofauti na wenye uamuzi wa kukabidhi lungu la mwenyekiti na makamu wake ni wabunge wa CCM ambao ni wengi kwenye kamati.
 
Hawa jamaa wanapigiwa kura na nani? Wabunge, au? Kama ni wabunge basi Cheyo wala hana upinzani wa kutisha kama ulivyoripoti unless wabunge wa CCM wawe wamebadilika!! Kwa ninavyofahamu upuuzi uliopo bungeni, usishangae wabunge wa CCM wakampigia Cheyo badala ya Zitto! Nakumbuka hata Uenyekiti kupitia POAC, inasemekana Zitto ilibidi apige magoti kwa JK baada ya wana-CCM kutaka kumtosa!
 
Kamati iliyokuwa ya ya Mrema nayo inahitaji mwenyekiti kutoka upinzani. Je, kama Mrema ametolewa, wajumbe wa kutoka upinzani katika kamti hiyo ni kina nani?
 
Mkuu, wanapigiwa na wajumbe walioteuliwa kuunda kamati hiyo and obvious, Wabunge wa CCM watakuwa ni wengi, subiri a minute nikupe majina yao
 
Hawa jamaa wanapigiwa kura na nani? Wabunge, au? Kama ni wabunge basi Cheyo wala hana upinzani wa kutisha kama ulivyoripoti unless wabunge wa CCM wawe wamebadilika!! Kwa ninavyofahamu upuuzi uliopo bungeni, usishangae wabunge wa CCM wakampigia Cheyo badala ya Zitto! Nakumbuka hata Uenyekiti kupitia POAC, inasemekana Zitto ilibidi apige magoti kwa JK baada ya wana-CCM kutaka kumtosa!

Mkuu, wanapigiwa na wajumbe walioteuliwa kuunda kamati hiyo and obvious, Wabunge wa CCM watakuwa ni wengi, wajumbe ndiyo hawa,
KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ___________________
1 Mhe. Deusiderius John Mipata, Mb
2 Mhe. Deo Haule Filikunjombe, Mb
3 Mhe. Asha Mshimba Jecha, Mb
4 Mhe. Lucy Philemon Owenya, Mb
5 Mhe.Ester Nicholas Matiko, Mb
6 Mhe. John Momose Cheyo, Mb
7 Mhe. Kabwe Zitto Zuberi, Mb
8 Mhe.Zainab Matitu Vulu, Mb
9 Mhe. Ally Keissy Mohamed, Mb
10 Mhe. Zainab Rashid Kawawa, Mb
11 Mhe. Kheri Ali Khamis, Mb
12 Mhe. Faida Mohamed Bakari, Mb
13 Mhe. Ismael Aden Rage,Mb
14 Mhe.Modestus Dickon Kilufi, Mb
15 Mhe. Abdul Jabir Marombwa, Mb
16 Mhe.Gaudence Casssian Kayombo, Mb
17 Mhe. Kombo Khamis Kombo, Mb
18 Mhe. Catherine Valentine Magige, Mb
 
Kamati iliyokuwa ya ya Mrema nayo inahitaji mwenyekiti kutoka upinzani. Je, kama Mrema ametolewa, wajumbe wa kutoka upinzani katika kamti hiyo ni kina nani?
Mkuu hawa ndiyo wajumbe wa kamati ya Hesabu za serikali za mitaa.

KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA ______________________________ _________
1 Mhe. Tauhida Cassian Galosi Nyimbo, Mb
2 Mhe. Dunstan Daniel Mkapa, Mb
3 Mhe. Azza Hillal Hamad, Mb
4 Mhe. Yahya Kassim Issa, Mb
5 Mhe. Menrad Lutengano Kigola,Mb
6 Mhe. Bahati Ali Abeid, Mb
7 Mhe. Kulthum Jumanne Mchuchuli, Mb
8 Mhe. Rajab Mbarouk Mohammed,Mb
9 Mhe. Yusuph Abdallah Nassir, Mb
10 Mhe. Philipa Geofrey Mturano, Mb
11 Mhe. Eustas Osler Katagira, Mb
12 Mhe. Muhonga Said Ruhwanywa, Mb
13 Mhe. Munde Tambwe Abdallah, Mb
14 Mhe. Ezekiel Magolyo Maige,Mb
15 Mhe. Mch. Israel Yohana Natse, Mb
16 Mhe. Alfaxard Kange Lugola, Mb
17 Mhe. Felista Aloyce Bura, Mb
18 Mhe.Suleiman Jumanne Zedi, Mb
 
?????!!!!! Haya mkuu, asante...
 
kamati zote muhimu(nishati,serikali za mitaa na pac(former poac))zimefanyiwa umafia ili madudu ya serikali yasiwekwe hadharani,zitto atapigwa chini na cheyo kwa msaada wa wa ccm..kumbe umafia wa ccm ni zaidi ya kutengeneza clip feki!!
 
Wanaong'ang'ania kuupata uenyekiti wa kamati ni kwa maslahi ya wananchi au maslahi binafsi, maana kuwa mjumbe wa kawaida tu kwenye kamati mchango wako si utasikika tu??kwa nn ugombanie uenyekiti wa kamati kwani jambo likishindikana si linaamuliwa kwa kura? au mwenyekiti ana allowances and marupurupu mengine zaidi ya wajumbe??
 
Mkuu, wanapigiwa na wajumbe walioteuliwa kuunda kamati hiyo and obvious, Wabunge wa CCM watakuwa ni wengi, wajumbe ndiyo hawa,
KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ___________________
Thanks for information. Naona timu yenyewe imekaa kichachama zaidi....anyway, labda wanaweza kuweka Utanzania mbele na kutoa chaguo sahihi litakalosimamia maslahi ya TZ.
 
Makinda atakumbukwa kwa kuharibu kila kitu na kukandamiza demokrasia bungeni!ndio makosa makubwa sana ya kupewa vyeo ambavyo hustahili...lazima uwe mtumwa!!
 
Wanaong'ang'ania kuupata uenyekiti wa kamati ni kwa maslahi ya wananchi au maslahi binafsi, maana kuwa mjumbe wa kawaida tu kwenye kamati mchango wako si utasikika tu??kwa nn ugombanie uenyekiti wa kamati kwani jambo likishindikana si linaamuliwa kwa kura? au mwenyekiti ana allowances and marupurupu mengine zaidi ya wajumbe??
Mkuu hapo umesema na kunigonga utosini.

Watu wameng'ang'ania mwenyekiti, mwenyekiti. Cha muhimu ni mbunge kuwepo kwenye hiyo kamati. Ukiona kuna kelele nyingi, kwa Tanzania, hii ni moja ya sign ya kuwepo maslahi fulani. Inashangaza kuna wabunge mpaka wanafanya kampeni za pesa. It's absurd.
 
Thanks for information. Naona timu yenyewe imekaa kichachama zaidi....anyway, labda wanaweza kuweka Utanzania mbele na kutoa chaguo sahihi litakalosimamia maslahi ya TZ.
Hiyo ndiyo swala/sala tunayoiomba sana.
 
kamati zote muhimu(nishati,serikali za mitaa na pac(former poac))zimefanyiwa umafia ili madudu ya serikali yasiwekwe hadharani,zitto atapigwa chini na cheyo kwa msaada wa wa ccm..kumbe umafia wa ccm ni zaidi ya kutengeneza clip feki!!

Mkuu binadamu akinyamazishwa mawe yatapiga kelele, kama njia rasmi zimezuiwa, njia mbadala zitatumika! Taarifa tutazipata tu!.
 
Naona wale wazee wa kuteteaa kila kitu hapa hawafika kabisaaa.
 
Mkuu hawa ndiyo wajumbe wa kamati ya Hesabu za serikali za mitaa.

KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA ______________________________ _________
1 Mhe. Tauhida Cassian Galosi Nyimbo, Mb
2 Mhe. Dunstan Daniel Mkapa, Mb
3 Mhe. Azza Hillal Hamad, Mb
4 Mhe. Yahya Kassim Issa, Mb
5 Mhe. Menrad Lutengano Kigola,Mb
6 Mhe. Bahati Ali Abeid, Mb
7 Mhe. Kulthum Jumanne Mchuchuli, Mb
8 Mhe. Rajab Mbarouk Mohammed,Mb
9 Mhe. Yusuph Abdallah Nassir, Mb
10 Mhe. Philipa Geofrey Mturano, Mb
11 Mhe. Eustas Osler Katagira, Mb
12 Mhe. Muhonga Said Ruhwanywa, Mb
13 Mhe. Munde Tambwe Abdallah, Mb
14 Mhe. Ezekiel Magolyo Maige,Mb
15 Mhe. Mch. Israel Yohana Natse, Mb
16 Mhe. Alfaxard Kange Lugola, Mb
17 Mhe. Felista Aloyce Bura, Mb
18 Mhe.Suleiman Jumanne Zedi, Mb

Hao wawili nafikiri ndo wabunge wa upinzani kwenye hii kamati. Sijui wana nguvu kiasi gani kwani TAMISEMI ndiko fedha nyingi na miradi mingi ya maendeleo inayowagusa wananchi moja kwa moja ilipo. Nani kati ya hawa anaweza kuisimamia TAMISEMI? Au kamati imedhoofishwa ili magamba waweze kupitisha hela kwa ajili ya kujiandaa na chaguzi zijazo?
 
Back
Top Bottom