MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 922
- 1,094
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba, atoa ufafanuzi kwa kamati kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara yake kwa Bajeti ya mwaka wa fedha wa uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.