Kamati ya bunge yampongeza Waziri Kairuki

kamati ya ufundi

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
416
439
b7ae340d4ae41c2415500bc54ffc280f.jpg

WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wamempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki kwa kusimamia vyema utendaji wa taasisi za umma zilizopo chini ya ofisi yake.

Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya Kairuki kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 kwa kamati hiyo.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, George Lubeleje alisema miongoni mwa eneo ambalo Waziri Kairuki anastahili pongezi ni la ukaguzi na usimamizi mzuri wa uhakiki wa kaya masikini zilizonufaika na fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini na kubaini kaya 63,813 zilizonufaika na mpango huo, huku zikiwa hazina sifa.

Pia, Lubeleje ambaye ni Mbunge wa Mpwapwa, alimpongeza waziri kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ambao kupitia mpango huo, serikali imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 1,068 na viongozi 219 wa vyama vya wakulima kutumia Hati za Haki Miliki za Kimila kukuza mitaji katika halmashauri za wilaya za Mwanga, Meru, Mbinga, Sumbawanga, Kalambo, Korogwe, Karagwe na Kilombero.
 
Wasisahau pia kumpongeza kwas uhakiki wa vyeti feki maana wengi wenye vyeti feki nasikia wamesha simamishiwa mishahara kuanzia mwezi january, february na wengine mwezi march hongera waziri.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom