jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,950
- 29,532
Habari zenu wakuu!
Leo tuitahadharishe kamati tajwa juu ya kuhakikisha afya ya mtanzania inaimarika kwa kuiwekea bajeti ya kutosha sekta ya afya kutoka kwenye mfuko wa hazina na sio kutegemea nyongeza ya mfuko wa wahisani.
Tumeshuhuduia sekta ya afya kuwa mojawapo ya sekta zilizotiwa msukosuko mkubwa na serikali pamoja na wananchi bila kuwa na mtetezi wa kuisemea.
Tumeshuhudia kelele za wanasiasa dhidi ya sekta hii bila hatua stahiki za kuongeza rasilimali.
Tumeshuhudia maonesho ya televisheni za makanjanja zikionesha uchakavu wa vitanda na sio ununizi wa vitanda vipya ...
Tumeshuhudia baadhi ya wabunge kujizolea ujiko kwa kuahidi misaada hewa kwenye vituo vya afya.
Hakuna aliyeongelea sana kwenye bajeti ya sekta ya afya katika ununuzi wa dawa au kulipa madeni ya watumishi waafya...
Upole wa watumishi wa sekta hii(wengi wao sio wanasiasa) umewafanya kuwa victim na scapegoat ya maamuzi mabovu ya vyombo vinavyoandaa na kuidhinisha bajeti.
Hakuna anayehoji juu ya kutopelekwa kwa fedha za miradi ya maendeleo ya sekta hii...hasa eneo la majengo ya huduma.
Wanasiasa wakubwa ...level ya ubunge wamejikuta wakiongelea kukosekana kwa panadol badala ya kukosekana kwa sera thabiti ya uchangiaji wa huduma za afya...Wanasiasa wanaimba kama chiriku juu ya afya bure kwa makundi flani huku fedha zote ni kwa hisani ya Watu wa Marekani n.k
sasa ni muda wa kamati hii kuubadili mfumo waafya kibajeti...
Tuachane na umbea wa kusema dawa zinaibiwa wakati dawa zenyewe zinaexpire zikiwa bohari ya madawa!!!
Nimeandika uzi huu baada ya kuwa inspired na taasisi ya SIKIKA ambayo imetuletea facts on table juu ya ufinyu wa bajeti kwa sekta hii.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!