Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,606
Kamati ya amani ya mkoa wa Mwanza imesema, kwa kushirikiana na serikali pamoja na viongozi wa dini zote nchini, itaendelea kutoa hamasa kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa uhuru na haki tarehe 29 Oktoba 2025, huku ikiwahimiza wananchi kutumia haki yao ya msingi kwenda kuchagua viongozi wanaowataka katika ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani.
Kamati hiyo imeeleza hayo katika tamko la pamoja lililotolewa leo Oktoba 20, 2025, baada ya kukamilika kwa kongamano la amani la viongozi wa dini mbalimbali lililofanyika mkoani Mwanza. “Tutaendelea kuhamasisha wananchi wa mkoa wa Mwanza na nchi nzima kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa uhuru na haki siku ya tarehe 29, Oktoba 2025.”
Imeeleza kamati hiyo. Kamati hiyo imewasisitiza wananchi kuwa baada ya zoezi la kupiga kura warudi katika makazi yao kwa utulivu, bila vurugu na maneno ya chuki, ili kudumisha taswira njema ya taifa.
Aidha, imebainisha kwamba itaendelea kuhakikisha inasimamia maombi katika kipindi chote cha uchaguzi, ikisisitiza kwamba jamii itambue kuwa amani ndiyo nguzo pekee ya maendeleo katika taifa.