Kamati ya Al Azhar na kuunda Qur’an standard (1924)

Kamati ya Al Azhar na kuunda Qur’an standard (1924)

Leo Quran inachukuliwa kuwa ni nakala moja tu inayosomwa na Waislamu duniani.

Lakini kihistoria, hapo awali Qur’an zilikuwa na tofauti kubwa si tofauti kidogo tu ya alama za vokali, bali maneno, aya, na hata sura zenye mpangilio tofauti.

Tukio la toleo la Cairo (1924) lilisawazisha historia hii na kuunda Qur’an inayotumika sasa, ikichukua nafasi ya maelfu ya misahafu tofauti iliyokuwa ikitumika Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, na sehemu za Asia.

Mwaka 1923–1924, Mfalme Fuad wa kwanza wa Misri aliona hitaji la kuwepo na toleo rasmi la Qur’an.

Alitoa maagizo ya kuunda kamati ya Al‑Azhar, inayojumuisha wanazuoni mashuhuri wa taasisi hiyo.

Waliotajwa katika kamati ni pamoja na
Muhammad b. ‘Ali al‑Husayni al‑Haddad
Sheikh Abdul Rahman al‑Sanusi
Sheikh Mustafa al‑Mahdi

Kazi yao ilikuwa
Kukusanya misahafu yote iliyokuwa ikitumika.
Kubaini tofauti kubwa za qira’at, aya, maneno, na sura.

Kisha Kusanifisha Qur’an moja yenye usomaji wa Hafs ‘an ‘Asim, ambayo sasa inatambulika duniani kote.

View attachment 3541618

Kabla ya standard ya Cairo ,Quran zilikuwa nyingi na kila mtu alikuwa anasoma anakuja na tafsiri,maana zake ,kila ukanda ulikuwa na Quran tofauti tofauti.

Tofauti zilizokuwepo ni

Njia 10 za qira’at:
kila njia ilisomwa tofauti, na baadhi ya Quran zilihesabu aya tofauti au kuacha baadhi ya aya.

Sura tofauti: mpangilio ulikuwa tofauti, hasa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Maneno tofauti: baadhi ya aya zilikuwa na maneno tofauti kabisa, ambayo yanayoweza kubadilisha maana ya mafundisho.

Ukosefu wa nakala thabiti: misahafu mingi haikuandikwa kwa uangalifu, baadhi ikapotea, ikasababisha mashaka kuhusu uthabiti wa maandiko.
Kumbuka Uthman alichoma misahafu yote moto ,hilo linajulikana na hakuna popote pale kipande cha Quran ya Uthman kilichopo duniani .

View attachment 3541619

Hii ni tofauti kubwa, si tofauti ndogo kama baadhi ya wanazuoni wanavyodai.,ili kuficha ukweli,

Mfalme Fuad na yeye akachoma misahafu yote na kuitupa kwenye Mto Nile .

Mfalme Fuad aliona misahafu ina makosa na tofauti ni kubwa hivo ni kuifuta na kuipoteza Kisha uundwe msahafu mmoja utakaotumika duniani kote.

Hii ilifanyika kabla ya kuanza kazi ya kusanifisha Qur’an mpya, toleo la Cairo, ambalo liliweka msingi wa usomaji mmoja rasmi.,ambao Leo waislamu wengi wasiojua chochote utasikia wanasema Quran haijawahi kubadilishwa ,Quran imeshushwa ,n.k

Ujue hizi dini Zina tabaka mbili ,wachache ndio wanapewa zile Siri za ndani, na wengi wanafichwa wanapewa maana za nje

Albert Pike, mmoja wa wanazuoni wakuu wa Freemasonry, anabainisha

“The symbols of the ancient religions were never intended to be understood by the multitude. They were vehicles of truth for the initiated alone.”
(Moral and Dogma of the Ancient and Accepted Scottish Rite of Freemasonry, Albert Pike, p. 15)

Anamaanisha

Alama za dini za kale hazikukusudiwa kueleweka na umma. Zilikuwa vyombo vya ukweli kwa wale waliopitishwa katika siri pekee.”
Pia Rudolf von Sebottendorff anafafanua mbinu kama hizi anasema

“Institutions can serve to conceal inner doctrines, providing a public front while preserving hidden teachings for the initiated.”
(Secret Practices of the Sufi Freemasons, p. 77)

Anamaanisha
“Taasisi zinaweza kutumika kuficha mafundisho ya ndani, zikitoa uso wa umma huku zikihifadhi mafundisho yaliyofichwa kwa waliopitishwa.

Kwahiyo hata hili swala la mchakato wa Quran kufanyiwa standardization,kuhaririwa na kupangiliwa vizuri pale Al Azhar University 1924 , huwezi kukuta linafundishwa madrasa ,ndio maana Kuna MASHEIKH mpaka wanakufa wao walishaaminishwa kuwa Quran ilishuka kutoka mbinguni, Quran ni hii ya karne ya 7, haijawahi kubadilishwa hata HERUFI.

Kwenye dini,Imani yoyote ile Kuna Esoteric meaning na Exoteric Meaning

Hata Yesu alizungumzia hili jambo akiwaambiwa wanafunzi wake ,kuwa wao wamepewa/wamejaariwa Siri za mbinguni ,

Sasa na kwenye Imani au dini au cult mfumo ni huo huo .

Exoteric (Zahir/Nje)
Ni tabaka la dini linaloonekana kwa waumini wote.
Hapa hupewa maana rahisi na wazi, kama ibada, sheria, mafunzo ya maadili, na mafundisho ya kawaida.
Lengo lake ni kuunda utaratibu wa kidini na maadili kwa jamii, kuhakikisha umma unafuata dini bila kuingiliwa na siri nzito.

Esoteric (Batin/Ndani)
Ni tabaka la siri, kwa wachache tu waliochaguliwa au waliopitia initiation.
Hapa hujifunza maana za ndani ya alama, symbols, namba, herufi, na rituals.
Lengo ni kuelewa mafumbo ya dini, cosmic order, na mchakato wa ufahamu wa kiroho.

Nitatoa mfano kidogo

Exoterically, Umma unaambiwa Jiwe Jeusi ni jiwe la baraka.

Esoterically, jiwe ni lugha, si kitu. Lugha haibadiliki kwa kubadilisha dini. Hapa ndipo Kaaba kama cube (mche) inaingia kwenye occult symbolism.

Manly P. Hall anaandika

The cube is the symbol of the material universe under law.”
(The Secret Teachings of All Ages, Manly P. Hall, p. 133)
Mche ni alama ya ulimwengu wa kimwili chini ya sheria.

Exoterically, Kaaba ni nyumba ya Mungu na ndio wengi sana wameaminishwa hivo.

Ila Esoterically, ni kitovu cha nidhamu, mwelekeo, na udhibiti wa mwili na fikra. Ndiyo maana mwili mzima wa Kiislamu unaelekezwa upande mmoja (Qibla), mara tano kwa siku, kwa mabilioni ya watu.

Huu si mpangilio wa kiholela; ni mfumo.

Ndani ya Freemasonry, jiwe linawakilisha mwanadamu mwenyewe.

Pike anaandika
“Man is a rough stone, and education is the process of polishing it.”
(Morals and Dogma, Albert Pike, p. 13)
Mwanadamu ni jiwe bovu, na elimu ndiyo mchakato wa kulisugua.
Kwenye Imani ,dini yoyote chunguza Kuna Esoteric na Exoteric Meaning

Tuendelee na mada yetu ya Mchakato wa Usanikishaji wa Quran,

Cha kushangaza Saudi Arabia, taifa lililochukuliwa kama kitovu cha Uislamu waliikataa standard ya Cairo hadi mwaka 1985 ndipo wakaikubali.

Kabla ya hapo, waliendelea kutumia qira’at nyingine na misahafu ambazo hazikufuata toleo la Hafs moja kwa moja.

Hii inadhihirisha kuwa hata ulimwengu wa Kiarabu haukukubali mara moja toleo la Cairo, jambo linaloshangaza.

Katika nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania, Qur’an zilikuwa na njia tofauti za qira’at hadi katikati ya karne ya 20.

Toleo la Hafs limekubaliwa rasmi na madhehebu yote ya Sunni, hasa shule za kidini na madrasa za Qur’an.
Hii inaonyesha kwamba toleo la Cairo limeleta mfumo mmoja wa Qur’an, lakini si mara moja au kirahisi tu.

Leo, mjadala huu mara nyingi huzuiwa au kufichwa,
Mifano ni ule mjadala ambao ulitikisa sana ulimwengu wa uislamu,ambapo Sheikh Mohammed Hijab na Qadhi walifanya huu mjadala YouTube,ikaleta mtikisiko mkubwa.

Baadae waliondoa ile video na wakasema

not suitable for the unlearned” (haifai kwa wasio na elimu)

Tunarudi pale pale kwenye ESOTERIC NA EXOTERIC MEANING

Kuna vitu vya kupewa maamuma na Kuna vitu vya wachache ,ndio maana mifumo yote ya dini, Imani imejengwa kwa mfumo wa PYRAMID

Wengi wanakuwa chini, wachache waliojuu ndio wanapewa Siri

Al Azhar University ni chuo ambacho tumeona kwa miaka mingi kikiwa kinashirikiana sana na Vatican ,ni chuo hicho hicho ndio kimehusika kuunda Quran,
The current Quran was written by Al-Azhar University in Egypt in 1924 under the patronage of King Fuad 1. It was amended by King Faruq in 1936. Pre-1924 Qurans were thrown into River Nile. In 2024 it marked 100 years since the current Quran HAFS was standardized. 👌

Kwa Leo niishie hapa.
Hawa huamini iliahushwa
 
🤣🤣🤣.yaani unatia hadi aibu.kwa hyo.nabii kwako ni nani na nani?
Mimi nitie aibu au wewe ambaye nimekwambia leta andiko la kuwa Nuhu ni nabii

Masaa 48 sasa hujaleta
 
Mimi nitie aibu au wewe ambaye nimekwambia leta andiko la kuwa Nuhu ni nabii

Masaa 48 sasa hujaleta
Unatia aibu Kwa sababu.hata maana ya nabii HAUJUI.
Wewe unadhani nuhu aliingiaje kwenye taurati ?au unadhani ngonjera zile
 
Mimi nitie aibu au wewe ambaye nimekwambia leta andiko la kuwa Nuhu ni nabii

Masaa 48 sasa hujaleta
Nimekupa Aya kwenye Quran.surat nuhu Aya 1 kwanza.mungu anasema TUMEMTUMA NUHU.
Bado unabisha
 

Attachments

  • Screenshot_20260221-211040.jpg
    Screenshot_20260221-211040.jpg
    161.5 KB · Views: 6
Back
Top Bottom