Kamati tano 5 bunge la katiba zakwama

Kamati tano 5 bunge la katiba zakwama

daniel merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
277
Reaction score
98
Kamati tano kati ya saba za Bunge Maalumu la Katiba zimejikuta katika njiapanda ya kushindwa kufanya maamuzi kutokana na kukosekana kwa akidi kwenye vikao vya kamati hizo. Kwa mujibu wa mjumbe mmojawapo wa Bunge hilo, Teddy Ladislaus, kukosekana kwa akidi katika kamati nyingi kumezifanya zishindwe kufanya maamuzi ikiwamo upigaji kura kwenye ibara mbalimbali. Ladislaus, ambaye ni kutoka kundi la 201 akiwakilisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, alisema mjadala ndani ya kamati hizo umekuwa mgumu na kamati zinashindwa kumaliza kazi kwa muda uliopangwa kutokana na kukosekana kwa akidi ya kuwezesha kufanya maamuzi kutokana na wajumbe kutohudhuria kwa sababu mbalimbali. Hadi sasa kati ya kamati saba zilizotoa maendeleo ya mjadala wa rasimu ya katiba ni kamati mbili pekee zilizopigwa kura katika kile kilichojadiliwa. Mwenyekiti wa Kamati namba moja, Ummy Mwalimu, juzi aliahidi kuwa upigaji kura ungefanyika siku hiyo baada ya kujadili sura nne za rasimu hiyo, lakini hadi sasa zoezi hilo halijafanyika. Aidha, Mwenyekiti wa kamati namba tano, Steven Wasira, akizungumza na NIPASHE alisema upigaji kura haujafanyika kwenye kamati yake licha ya kujadili sura ya pili, tatu, nne na tano. Kamati zilizotoa mrejesho wa majadiliano yao hadi sasa ni namba 9, 10, 11, 12, ambazo hazijaeleza kama wamepiga kura, huku kamati namba tatu wakipiga kura na kuwa na maoni ya wengi na wachache. ATAKA BUNGE LIAHIRISHWE Katika hatua nyingine, Ladislaus alisema viongozi wakuu wanapaswa kutambua kuwa katiba bora itapatikana kwa maridhiano na siyo kwa ushindani na ubabe wa kisiasa. Aidha, alisema vilevile kuwa ni vyema bunge hilo likaahirishwa kwa kuwa hivi sasa, kamati zinajadili sura za rasimu ya katiba kwa muundo wa "bora liende" na hakuna matumaini ya kupata katiba mpya yenye misingi ya umoja wa kitaifa. Ladislaus aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa ni vyema Rais akaona umuhimu wa kusitisha shughuli za Bunge hilo kwa sasa na kutafuta maridhiano ya pande zinazovutana. Mjumbe huyo, ambaye katika mkutano huo alikuwa ameambatana na Rais Mstaafu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Hemed Mngwali na Mwanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma (ARDP), Elisante Mfinanga, alisema tamko analolitoa ni kwa niaba ya wanafunzi wa vyuo vikuu anaowawakilisha ndani ya bunge la katiba. Alisema kuwa hadi sasa, Bunge hilo lipo katika mkwamo mkubwa kwani licha ya kamati kuendelea na uchambuzi wa rasimu, ukweli ni kwamba (wajumbe) wanapata ugumu kufikia akidi ya kuwezesha vikao kufanya maamuzi na kukidhi matakwa ya sheria ya mabadiliko ya katiba. "Kamati za Bunge Maalum zinaendelea na uchambuzi wa Rasimu ya Katiba, lakini ni kweli kwamba uchambuzi huu wa sasa hauwezi kutuletea katiba bora inayokusudiwa na Rais Jakaya Kikwete... muda wa siku 16 kujadili sura 15 zenye ibara 240 ikiwa ni wastani wa ibara 16 kwa siku moja kazi haitafanyika kwa weledi," alisema. Mjumbe huyo alitoa maoni yaliyoungwa na wenzake, akisema kuwa ni vyema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakaloketi Novemba mwaka huu kufanya marekebisho kwenye katiba ya sasa ya mwaka 1977 kwa kuweka vipengele vya kuwapo kwa tume huru ya uchaguzi, haki ya kuhoji matokeo ya urais na kuwapo kwa mgombea binafsi. Aliongeza kuwa, kuendelea kuharakisha mchakato wa kutengeneza Katiba kwa namna inayoendelea sasa hakutaleta katiba bora kwani haitakuwa na ridhaa ya makundi mengi kwenye jamii. UGUMU KWENYE KAMATI Ladislaus alibainisha kuwa kwa kadri anavyoona, hivi sasa kamati za Bunge Maalum la Katiba zimekuwa zikifanya kazi alimradi tu kufika mwisho na ionekane kwamba kazi ya kupata katiba mpya imefanyika, jambo analoamini kuwa ni dhambi kubwa kwani kufanya hivyo ni kuhadaa mamilioni ya Watanzania kuwa watapatiwa katiba bora wakati hilo halitawezekana bila pande zote zinazovutana kufikia maridhiano. "Kwa kuwa Katiba ni moyo wa nchi, tusifanye kazi kwa kulipua alimradi tuwapendeze wachache walioweka maslahi binafsi mbele.Tukifanya hivyo tutakuwa tunaliweka taifa rehani ... na baadaye taifa litaachwa liharibike mikononi mwetu sisi vijana," alisema. Akielezea kuhusu haja ya kuwapo kwa mazungumzo baina ya CCM na Ukawa, Ladislaus alisema: "Mazunguzo siku zote ni 'give and take' yaani kulegeza msimamo katika baadhi ya hoja badala ya kila upande kushupaa kwa kile unachokiamini, tukiwa na nia ya dhati ya kuzungumza, tukashauriana, tukaridhiana na kukubaliana jinsi ya kutekeleza yale tulioafikiana, basi Taifa litapata Katiba bora hivyo kuondoka katika mkwamo wa sasa na kuondoa mgawanyiko," alisema. Ukawa huundwa na wajumbe kutoka vyama vikuu vya upinzani nchini vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi. Wajumbe wa Ukawa walisusia vikao vya Bunge Maalum la Katiba tangu April 16, 2014, ikiwa zimebaki siku 10 Bunge hilo kuhairishwa na wameweka msimamo wa kutorejea tena Bungeni hadi litakapojikita kwenye kujadili Rasimu ya wananchi iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Chanzo: Nipashe
 
Kamati tano kati ya saba za Bunge Maalumu la Katiba zimejikuta katika njiapanda ya kushindwa kufanya maamuzi kutokana na kukosekana kwa akidi kwenye vikao vya kamati hizo. Kwa mujibu wa mjumbe mmojawapo wa Bunge hilo, Teddy Ladislaus, kukosekana kwa akidi katika kamati nyingi kumezifanya zishindwe kufanya maamuzi ikiwamo upigaji kura kwenye ibara mbalimbali. Ladislaus, ambaye ni kutoka kundi la 201 akiwakilisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, alisema mjadala ndani ya kamati hizo umekuwa mgumu na kamati zinashindwa kumaliza kazi kwa muda uliopangwa kutokana na kukosekana kwa akidi ya kuwezesha kufanya maamuzi kutokana na wajumbe kutohudhuria kwa sababu mbalimbali. Hadi sasa kati ya kamati saba zilizotoa maendeleo ya mjadala wa rasimu ya katiba ni kamati mbili pekee zilizopigwa kura katika kile kilichojadiliwa. Mwenyekiti wa Kamati namba moja, Ummy Mwalimu, juzi aliahidi kuwa upigaji kura ungefanyika siku hiyo baada ya kujadili sura nne za rasimu hiyo, lakini hadi sasa zoezi hilo halijafanyika. Aidha, Mwenyekiti wa kamati namba tano, Steven Wasira, akizungumza na NIPASHE alisema upigaji kura haujafanyika kwenye kamati yake licha ya kujadili sura ya pili, tatu, nne na tano. Kamati zilizotoa mrejesho wa majadiliano yao hadi sasa ni namba 9, 10, 11, 12, ambazo hazijaeleza kama wamepiga kura, huku kamati namba tatu wakipiga kura na kuwa na maoni ya wengi na wachache. ATAKA BUNGE LIAHIRISHWE Katika hatua nyingine, Ladislaus alisema viongozi wakuu wanapaswa kutambua kuwa katiba bora itapatikana kwa maridhiano na siyo kwa ushindani na ubabe wa kisiasa. Aidha, alisema vilevile kuwa ni vyema bunge hilo likaahirishwa kwa kuwa hivi sasa, kamati zinajadili sura za rasimu ya katiba kwa muundo wa "bora liende" na hakuna matumaini ya kupata katiba mpya yenye misingi ya umoja wa kitaifa. Ladislaus aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa ni vyema Rais akaona umuhimu wa kusitisha shughuli za Bunge hilo kwa sasa na kutafuta maridhiano ya pande zinazovutana. Mjumbe huyo, ambaye katika mkutano huo alikuwa ameambatana na Rais Mstaafu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Hemed Mngwali na Mwanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma (ARDP), Elisante Mfinanga, alisema tamko analolitoa ni kwa niaba ya wanafunzi wa vyuo vikuu anaowawakilisha ndani ya bunge la katiba. Alisema kuwa hadi sasa, Bunge hilo lipo katika mkwamo mkubwa kwani licha ya kamati kuendelea na uchambuzi wa rasimu, ukweli ni kwamba (wajumbe) wanapata ugumu kufikia akidi ya kuwezesha vikao kufanya maamuzi na kukidhi matakwa ya sheria ya mabadiliko ya katiba. "Kamati za Bunge Maalum zinaendelea na uchambuzi wa Rasimu ya Katiba, lakini ni kweli kwamba uchambuzi huu wa sasa hauwezi kutuletea katiba bora inayokusudiwa na Rais Jakaya Kikwete... muda wa siku 16 kujadili sura 15 zenye ibara 240 ikiwa ni wastani wa ibara 16 kwa siku moja kazi haitafanyika kwa weledi," alisema. Mjumbe huyo alitoa maoni yaliyoungwa na wenzake, akisema kuwa ni vyema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakaloketi Novemba mwaka huu kufanya marekebisho kwenye katiba ya sasa ya mwaka 1977 kwa kuweka vipengele vya kuwapo kwa tume huru ya uchaguzi, haki ya kuhoji matokeo ya urais na kuwapo kwa mgombea binafsi. Aliongeza kuwa, kuendelea kuharakisha mchakato wa kutengeneza Katiba kwa namna inayoendelea sasa hakutaleta katiba bora kwani haitakuwa na ridhaa ya makundi mengi kwenye jamii. UGUMU KWENYE KAMATI Ladislaus alibainisha kuwa kwa kadri anavyoona, hivi sasa kamati za Bunge Maalum la Katiba zimekuwa zikifanya kazi alimradi tu kufika mwisho na ionekane kwamba kazi ya kupata katiba mpya imefanyika, jambo analoamini kuwa ni dhambi kubwa kwani kufanya hivyo ni kuhadaa mamilioni ya Watanzania kuwa watapatiwa katiba bora wakati hilo halitawezekana bila pande zote zinazovutana kufikia maridhiano. "Kwa kuwa Katiba ni moyo wa nchi, tusifanye kazi kwa kulipua alimradi tuwapendeze wachache walioweka maslahi binafsi mbele.Tukifanya hivyo tutakuwa tunaliweka taifa rehani ... na baadaye taifa litaachwa liharibike mikononi mwetu sisi vijana," alisema. Akielezea kuhusu haja ya kuwapo kwa mazungumzo baina ya CCM na Ukawa, Ladislaus alisema: "Mazunguzo siku zote ni 'give and take' yaani kulegeza msimamo katika baadhi ya hoja badala ya kila upande kushupaa kwa kile unachokiamini, tukiwa na nia ya dhati ya kuzungumza, tukashauriana, tukaridhiana na kukubaliana jinsi ya kutekeleza yale tulioafikiana, basi Taifa litapata Katiba bora hivyo kuondoka katika mkwamo wa sasa na kuondoa mgawanyiko," alisema. Ukawa huundwa na wajumbe kutoka vyama vikuu vya upinzani nchini vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi. Wajumbe wa Ukawa walisusia vikao vya Bunge Maalum la Katiba tangu April 16, 2014, ikiwa zimebaki siku 10 Bunge hilo kuhairishwa na wameweka msimamo wa kutorejea tena Bungeni hadi litakapojikita kwenye kujadili Rasimu ya wananchi iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa maoni yangu kile kilichoandikwa na ----- jana kwamba kinachomtesa sitta ni MIL 150 ni kweli,Jna kwenye taarifa ya habari ITV kiongozi mmoja wa kamati alisema wabunge wanafika wana sign posho na kuondoka haya manyang'ahu hayawezi leta katiba ya wananchi. tatizo wanataka posho za kuhonga uchaguzi wa serikali za mitaa na 2015 Imeandikwa na Salome Kitomari, Editha Majura na Godfrey Mushi, Dodoma CHANZO: NIPASHE

Huyu bwana mdogo amesema ukweli kabisa na anaitendea haki nafsi yake. Siyo kweli kwamba wajumbe walioko Dodoma wanaandika rasimu mpya bali wako huko kupokea posho za bure.
Katiba mpya inatakiwa kuwaleta wananchi pamoja na kuponya majeraha yao lakini kinachofanyika Dodoma ni kuandika katiba itakayoleta mpasuko katika jamii.Utaandikaje sheria mama ya nchi huku kundi kubwa liko nje likilalamikia rafu inayofanywa na chama tawala?
Chukulia mfano juzi wakati mwenyekiti wa BMK alipokutana na wafugaji.Atafanyaje hivyo wakati yeye ni mwenyekiti wa BMK ambalo ni la muungano wakati wizara ya mifugo si ya muungano? Je,wafugaji hao waliwawakilisha pia wafugaji wa Zanzibar? Ndio maana tunasema serikali tatu haikwepeki.
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.
 
Awatafanikiwa akina wassira na lukuvi

mama hapa katiba prof. wako aende ze komedi
 
Nampenda sana Prf Tibaijuka, lakn ni dikteta, hawezI kuiongoza nchi hii
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.

Yule ni fisadi namba moja! Tena fisadi mwanamke ni wa kumuogopa kama ukoma.
 
Huyu binti ameongea vema lakini maajabu yake atakuja kupiga kura ya kuipinga rasimu ya warioba! Nategemea hatafanya hivyo!
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.
Kuna uhusiano gani wa mada na ulichokiekeza hapa kuhusu Tabaijuka? Huyu Prof si alishindwa kazi huko alikokuwa. Kwa taarifa yako prof hawezi kuwa kiongozi mzuri, mifano tunayo, huyo tibuijuka ni bomu
 
Hakuna cha Anna Tibaijuka wala nan tunahitaj rais strong kwaajil ya maslah ya watanzania sio tu et kisa professor, I ts true tunahitaj mtu with reasonable education kutokana na ulimwengu wa sasa,, but uzalendo kwa nchi yetu ndo jambo la msing.
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.

Utahangaika sana wewe mama kujipigia debe!!
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.

Utafiti huo ulifanywa na Taasisi gani na lini? Na matokeo ya utafiti huo yanapatikana wapi?
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.

Kama uzoefu wa kimataifa ungalikuwa dawa, JK asingaliangukia pua
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.
Toa ujinga wako ma huyo rais wako mwanamke! kwenye mambo ya msingi! si tunaumizwa huku wewe unaongea maujinga
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.
hili ni li spinn doctor hamuoni kwa muda mchache tu limefanikiwa kuhamisha mjadala
 
Back
Top Bottom