Kamati maalum ya vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Dar yateuliwa

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
879
969
*KAMATI MAALUM UVCCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA DSM YATEULIWA*

Mkuu Wa Idara Ya Vyuo Na Vyuo vikuu (UVCCM) Taifa Ndugu Daniel Zenda Leo Tarehe 3/05/2017 Amekutana na Kufanya Kikao Na Wenyeviti Na Makatibu Wa Matawi 32 Ya UVCCM Vyuo Na Vyuo Vikuu Dar Es salaam.

Mwenyekiti Wa kikao Na Mkuu wa Idara ya Vyuo Na vyuo Vikuu (UVCCM) Aliwaeleza Wajumbe Wa Kikao Hicho Ajenda Kuu ya Kuundwa Kwa Kamati Ambayo Itakuwa Chini Ya Usimamizi Wa Umoja Wa Vijana Wa CCM Mkoa Wa Dar Es Salaam.

Aidha Kamati Hiyo Itaratibu Masuala Yote Ya Kiutendaji Vyuo Na Vyuo Vikuu (UVCCM) Mkoa Wa Dar es Salaam Mpaka Hapo Uongozi Wa Mkoa Utakapochaguliwa

Baadhi ya Majukumu Ambayo kikao iliazimia Kusimamiwa na Kamati hiyo ni Pamoja na Masuala Yafuatayo:-

>Kamati Itashughulika Na Masuala Ya Uchaguzi Wa Matawi Ya UVCCM Vyuo Na Vyuo Vikuu

>Kamati Itashughulika Na Masuala Ya Mahafali Ya UVCCM Vyuo Na Vyuo Vikuu

>Kamati Itashughulika Na Masuala Yote Ya Mikutano Na Makongamano Yote Ya UVCCM Vyuo Na Vyuo Vikuu

Kamati Hiyo Ya Vyuo Na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa Wa Dar es Salaam Iliyoundwa Na Kikao Halali Hivi Leo Itaongozwa Na :-

*MWENYEKITI WA KAMATI*
Asha Feruzi
Chuo (Taasisi Watu Wazima)

*KATIBU WA KAMATI*
Geofrey A Kololo
Chuo (Muhimbili)

*KATIBU HAMASA WA KAMATI*
Bulugu Magege
Chuo (Mwl Nyerere)

*MJUMBE WA KAMATI*
James Shadrack
Chuo (DUCE)

*MJUMBE WA KAMATI*
Ally Mohamed Ummi
Chuo ( St Joseph)

*MJUMBE WA KAMATI*
Ameir Ali
Chuo (Diplomasia)

MJUMBE WA KAMATI
Abdulatif. B .Nkenda
Chuo (Bagamoyo)

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
IMG_20170503_211051_388.jpg
 
Kwenye heading ungeweka kabisa uvccm ili wadau wajue kuwa ni kamati ya kitu gani, maana ni ishu ya wachache hiyo waliobahatika kufika kwenye meza ya national cake
 
Hao sasa wanafukuzia digrii zao vyuoni, wakifika kuwa ma RC na DC utaambiwa wanajua kusoma na kuandika tu.

Haya yote yapo Tz tu.
 
Back
Top Bottom