Kamati Kuu ya CHADEMA, itakutana Mjini Dodoma katika kikao chake kuanzia Mei 12-13

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kuwa Kamati Kuu ya Chama itakutana Mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei 12-13.

Kikao hicho, pamoja na masuala mengine, kitajadili kwa kina taarifa ya hali ya siasa nchini sambamba na mwenendo wa Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ambayo imetimiza miezi 6 madarakani.

Aidha kikao hicho cha KK cha siku mbili, kitajadili na kupitisha Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka huu (kutokana na Mpango Mkakati wa Chama wa miaka 5) kabla ya Sekretarieti kuanza utekelezaji, ambao utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi.

Imetolewa leo Jumanne, Mei 10, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 

Attachments

  • TAARIFA- KK CC MEI .doc
    41.5 KB · Views: 101
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kujadili mwenendo wa utawala wa Rais John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa mchana huu kwa vyombo vya habari na Tumaini Makene, Afisa Habari wa Chadema inasema Kamati Kuu ya Chama itakutana Mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei 12-1.

“Pamoja na masuala mengine, kitajadili kwa kina taarifa ya hali ya siasa nchini Sambamba na mwenendo wa Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ambayo imetimiza miezi 6 madarakani,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, kikao hicho, kitajadili na kupitisha mpango kazi wa chama hicho kwa mwaka huu ambao unatokana na mpango mkakati wa chama wa miaka mitano.

“Kabla ya Sekretarieti kuanza utekelezaji, ambao utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi,” imesema taarifa hiyo.
 
awamu hii ni butua butua mpira hautulizwi na kupiga pasi za kueleweka uwanja nao unazidi kaharibika nyasi zinazid kuumia tu
 
Waje na ukosoaji wenye afya kwa Taifa.Hatutaki siasa uchwara.Na si wao tu,hata wale kijani na njano;wasituletee matamko yao ya siàsa uchwara.
 
Kwa ushauri tu nikufahamishe Chadema hawafanyagi Maigizo
Huo si ukweli, walikuja na mwembe yanga kukoga nyoyo za wananchi wakaishia kuwachukua waliowachafua. Siasa za CCM na CDM hazina tofauti maana ni wale wale walilelewa na CCM wakaingia upinzani kupata ruzuku kama Nyerer alivyokwisha sema.
 
Bila shaka mwenye chama mh.Laigwanani mkuu atahudhuria

Ingawa si mjumbe lakini kwa kuwa ni mmiliki atahudhuria.
 
Ukawa wasaidieni Ccm jinsi ya kutawala maana wameshachoka.. Chama chakavu kimeishiwa pumzi..
 
ivi Makene kazi yake huwa ni kutangaza mikutano ya kamati kuu tu....ni kama vile idara ya habari CDM imekufa...

He needs to gauge himself if he is still fit and relevant for the position

Sioni ubunifu katika idara hii ...poleni CDM naona mnazama mdogo mdogo
 
Daah kweli CDM is increasing at decreasing rate.....masaa matano yamepita tangu uzi huu ubandikwe....na hii ni post ya 15....huko nyuma hapa JF haikuwa hivyo
 
Daah kweli CDM is increasing at decreasing rate.....masaa matano yamepita tangu uzi huu ubandikwe....na hii ni post ya 15....huko nyuma hapa JF haikuwa hivyo

Mada hii inajadiliwa nini wakati ni tangazo? Fikra za ajabu kweli! Nyie ndio mnaoona msiba mzito ni ule wenye vilio vingi bila kujua siku hizi Waliaji wanakodiwa
 
Ulivyo chumbiwa ndiye alikuwa mshenga?
Askofu Josephat Gwajima amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa kuwa alishiriki kama ‘mshenga’ kumshawishi mwanasiasa huyo kumpokea Edward Lowassa katika chama hicho.Jana, Dk. Slaa alimtaja Askofu Gwajima kama mshenga.

Ukifika nyumbani mwambie bi mkubwa wako akuonyeshe picha zake za kitchen party utamuona Ritz pembeni yupo na mshenga.

Usisahu sawa.
 
Back
Top Bottom