GAMBLER
JF-Expert Member
- Nov 22, 2009
- 303
- 12
Nataraji humu jamvini hakuna mcheza kamari, na ninakushaurini msije mkajaribu huu mchezo, kwani addiction yake ni ngumu kuachika, na madhara yake ni makubwa sana. Binafsi nimeanza kucheza kamari miaka 10 ilopita.
Kabla sijauanza huu mchezo nilikuwa na very good life, nilikuwa na mke mzuri, lakini akanikimbia, nimejaribu kuoa mke mwingine naye pia akanikimbia. Nitajaribu kutaja baadhi ya matatizo niliyokumbana nayo katika kamari:-
1- Pesa zote huishia katika kamari.
2- Kutokuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa.
3- Kupungukiwa na nguvu za kiume.
4- Kutokuwa na furaha na amani.
5- Kuwa na madeni .
6- Kutoaminika na kukosa heshima katika jamii.
7- Kutoelewana na ndugu.
8- n.k..
Ninaomba kutoka kwenu, yeyote mwenye ushauri, au njia gani nitumie ambayo itanisaidia kupunguza kucheza, au kuachana nao kabisa huu mchezo.