Kamari! Kamari! Kamari!

Kamari! Kamari! Kamari!

GAMBLER

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2009
Posts
303
Reaction score
12
Nataraji humu jamvini hakuna mcheza kamari, na ninakushaurini msije mkajaribu huu mchezo, kwani addiction yake ni ngumu kuachika, na madhara yake ni makubwa sana. Binafsi nimeanza kucheza kamari miaka 10 ilopita.

Kabla sijauanza huu mchezo nilikuwa na very good life, nilikuwa na mke mzuri, lakini akanikimbia, nimejaribu kuoa mke mwingine naye pia akanikimbia. Nitajaribu kutaja baadhi ya matatizo niliyokumbana nayo katika kamari:-

1- Pesa zote huishia katika kamari.
2- Kutokuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa.
3- Kupungukiwa na nguvu za kiume.
4- Kutokuwa na furaha na amani.
5- Kuwa na madeni .
6- Kutoaminika na kukosa heshima katika jamii.
7- Kutoelewana na ndugu.
8- n.k..

Ninaomba kutoka kwenu, yeyote mwenye ushauri, au njia gani nitumie ambayo itanisaidia kupunguza kucheza, au kuachana nao kabisa huu mchezo.
 
pole sana na yaliyokusibu, mimi ningekushauri uende kwa kakobe ufanyiwe maombezi., subiri na wengine humu jamvini watakupa ushauri mzuri zaidi
 
Njia nzuri ya kutatua tatizo ni kurejea njia uliyoingia nayo,jaribu kutatua tatizo lililokufanya hadi ukaingia kwenye kamari
 
Kwanza,Hongera kwa kujua madhara ya kamari. Yaani hapo umeshatatua nusu ya tatizo.
Pili, sasa anza kuepukana na marafiki au maeneo unayocheza kamari.
Tatu, anza kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa dhati!
 
Wewe endelea tu na kamari zako ungeomba ushauri kabla hujaanza kucheza hapo ingekuwa vizuri
 
wana jf michango yenu inahitajika hapa, cause hata mimi kuna ndugu yangu ameathirika na kamari
 
unajua ukisha jua tatizo basi tiba inakuwa rahisi cha msingi hapo ni kuambia ubongo kuwa kamari basi na itakuwa basi kweli,ila hao wanaosema mara kwakakobe sijui usipite karibu na eneo no,feeling zako emotion ndizo zinazokupeleka huko we delete kabisa kwenye diskette yako,na utafanikiwa pia dharau huo mchezo watu naanachana na wapenzi wao sebuse hili!
 
Yeah hii kitu ni addictive mno lakini naona imekunasa pabaya mjomba. Inaonekana uliingia vibaya hii kitu. Kanuni ya kwanza kwenye kamali ni kwamba dont gamble what you can not afford to loose. Sasa mwenzetu naona una-gamble mpaka na ndoa zako hatari hii pumzika kwanza na toa ndoto za ukishinda utafanya nini.

Muhimu ni kwamba you can still enjoy gambling like i do responsibly, hila lazima uelewe kuna kupata na kukosa from the beggining. Hivyo do not put your expectations too high and set a limit i know its hard but you have to give priorities to life obligations too. Its very important you sort your personal life, have a clear direction and a purpose to life first those are what matters to you the most. Then you can gamble responsibly knowing whatever you put at the bookies if its gone doesnt affect the aftermath.

Remember the odds are always against you, hivyo wajamaa kama unawachangia tuu. I remember at the beggining of the season i had ten teams all won but Man-Utd got beaten by Burnley kwa kweli ulikua usiku mmbaya sana kwangu, the pot they costed me we acha tu kwa kweli. Hivyo lazima uende na high hopes of losing than winning utajikuta tabia inabadilika na kuanza kuangalia maisha vingine tena.
 
Nakupongeza sana mkuu kwa kuwa unawajali wengine. Wengi huwa wanapenda wakikwama wao basi waone na wengine wanaingia matatizoni. Hakuna njia nyingine mkuu isipokuwa kutafuta kazi mbadala itakayokukeep busy wakati wote. kucheza kamali mara nyingi kunatokana na kukosa shughuli ya msingi ya kufanya. Iwapo utajitafutia kazi inayoweza kukufanya uwe busy, utajikuta taratibu unaanza kupunguza umhimu wa kamari na kuingia kwenye hiyo kazi nyingine. Lakini challenge ya hili pia, ni je utapata wapi kazi na kazi gani?
 
Kwanza,Hongera kwa kujua madhara ya kamari. Yaani hapo umeshatatua nusu ya tatizo.
Pili, sasa anza kuepukana na marafiki au maeneo unayocheza kamari.
Tatu, anza kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa dhati!

NO NO NOOOO.....anza na namba tatu!!!! ......shit......
 
Yeah hii kitu ni addictive mno lakini naona imekunasa pabaya mjomba. Inaonekana uliingia vibaya hii kitu. Kanuni ya kwanza kwenye kamali ni kwamba dont gamble what you can not afford to loose. Sasa mwenzetu naona una-gamble mpaka na ndoa zako hatari hii pumzika kwanza na toa ndoto za ukishinda utafanya nini.

Muhimu ni kwamba you can still enjoy gambling like i do responsibly, hila lazima uelewe kuna kupata na kukosa from the beggining. Hivyo do not put your expectations too high and set a limit i know its hard but you have to give priorities to life obligations too. Its very important you sort your personal life, have a clear direction and a purpose to life first those are what matters to you the most. Then you can gamble responsibly knowing whatever you put at the bookies if its gone doesnt affect the aftermath.

Remember the odds are always against you, hivyo wajamaa kama unawachangia tuu. I remember at the beggining of the season i had ten teams all won but Man-Utd got beaten by Burnley kwa kweli ulikua usiku mmbaya sana kwangu, the pot they costed me we acha tu kwa kweli. Hivyo lazima uende na high hopes of losing than winning utajikuta tabia inabadilika na kuanza kuangalia maisha vingine tena.
ushauri wako ni bomba, pole sana burnley kakuua
 
Njia pekee ya kuacha kucheza huu mchezo ni,kuchukua hela yako yote kwenye account if any,na kuchezea kamali mpaka ziishe ndo utapata akili ya kutafuta nyingine na kutumia kwa uangalifu,kila ukikumbuka kilichotokea hautarudia tena huu mchezo!!
 
Kamari ya kekundu na keusi imekuwa ikichezwa sokoni Nyakanazi na watu wamekuwa wakiibiwa wakati vyombo vya usalama wakiona.

Je, kamari inaruhusiwa?
 
Kamari ya kekundu na keusi imekuwa ikichezwa sokoni Nyakanazi na watu wamekuwa wakiibiwa wakati vyombo vya usalama wakiona.

Je, kamari inaruhusiwa?

Wanasiasa washaingiza siasa
 
Kwa mazingira yaliyopo,kamari watawala wetu WAMEIRUHUSU.Labda ni mazingira tu ya kuchezea ndio tofauti.Premier betting,meridian betting,sport betting n.k. zote ni kampuni za kamari,tena wanatambuliwa rasmi na Serikali.
 
Toka ningali mdogo mamangu alinambia "hakuna maisha mazuri bila elimu" ila nimekua machizi wakanishauri "ili utoke kimaisha usiache kamari" na nikweli kamari inajenga,ofisi zinadumaza akili
 
Back
Top Bottom