Kamanda Sirro: Nasumbuliwa sana na wanawake usiku

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, amesema miongoni mwa changamoto anazokutana nazo ni pamoja kupigiwa simu za vishawishi na wanawake hasa usiku wa manane, wakidhani anapata pesa nyingi kwenye kazi yake.


Kamishna Sirro afichua siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, ambapo amesema pamoja na changamoto hizo, anajitahidi kukabiliana nazo kwa kuwa tayari amekwishawazoea.


Amesema kuna wanawake wengine wakiona amependeza kwenye tukio fulani, wanajua lazima atakuwa na pesa za kuwasaidia katika maisha yao hivyo wakati mwingine humpigia usiku, na yeye akidhani kuwa ni taarifa za uhalifu, lakini hukutana na vishawishi vikiambatana na sifa kedekede.


"Mwigine anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini, wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi". Amesema Kamanda Sirro


Sirro ametaja changamoto nyingine ambazo hukutana nazo kuwa ni pamoja na suala la askari wake kulalamikiwa jambo linaloonesha dhahiri kama kiongozi ameshindwa kuwasimamia vijana anaowaongoza na mara nyingi huwa anachukua hatua.


Lingine ni uhalifu kuzidi katika eneo fulani na hufanya wananchi kuwa na uoga, na kupoteza imani kwa jeshi la polisi jambo ambalo linamfanya yeye ajisikie vibaya zaidi kuliko hata wananchi, huku nyingine ikiwa ni viongozi wa mitaa kutowajibika katika kudhibiti uhalifu pamoja na kuletewa.
 
"Mwigine anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini, wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi". Amesema Kamanda Sirro


Kama amefikia hatua ya kutaniwa kiasi hicho maana yake yupo loose na he is not the right fit for the post, may be apewe nafasi ya u jaji wa mashindano wa mamiss
 
Sirro nae keshaivaa tabia ya Makonda.
Half mbona kama Siro anaonekana umri umeenda enda ,inakuaje anaongea upuuzi kama Huo kwenye media?

Hiyo changamoto ya wanawake asingeisema ingekua busara zaidi,haina mantiki kabisa
Uongozi wa dar sass unatia aibu, kuna mambo hupaswi kumwambia mtu licha kuongea kwenye midia.
Mwanaume lazima uwe na ghala pana kifuani ili kuhifadhi mambo
 
Back
Top Bottom