Kamanda Sirro anafanya kazi kwa shida

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,695
Haihitaji kuwa na degree ya uzamivu kujua kwamba kamanda Simon Sirro anatekeleza majukumu yake kwa shida. Historia yake, makuzi yake, wajihi wake vyote vinakuonyesha kwamba kamanda huyo anatekeleza wajukumu yake ya ukamanda kwa shida sana na si ajabu anaomba muda uende haraka astaafu akapumzike.

1. Akiwa amesoma seminari ni wazi amri kumi za Mungu anazijua na kuziimba kama ndege na hasa amri ya 7, katika kutekeleza majukumu yake ya ukamanda inabidi tu saa ingine aseme uongo hii inamuumiza sana.

2.Kazi ya U-polisi ameisomea na akafaulu vizuri course zote , sheria anazijua, katiba anaijua vilivyo, katika kutekeleza majukumu yake ya ukamanda inabidi afumbe macho na kupindisha sheria na saa ingine kuvunja katiba mfano kumweka mtu rumande zaidi ya masaa 24 bila kumfikisha mahakamani au kunyima watu vibali kufanya maandamano ya amani kama katiba inavyoruhusu au kufanya mikutano ya hadhara kama katiba inavyoruhusu si kwamba hajui ila basi afanyeje zaidi ya kumtumkia kafiri upate mradi wako.

3. Kufanya kazi na bosi kijana ambaye ana madaraka makubwa na ambae ana kila dalili ya kulewa madaraka lakini Kamanda Sirro ambaye wajihi wake una kila dalili za vielelezo vya weledi ina hitaji moyo, moyo kweli kweli, kamanda Sirro anaumia sana moyoni bosi kijana anavyowakosea adabu watu kwa makundi mbali mbali kwa mfano wabunge, kuwafokea watumishi wa serikali ambao wamemzidi umri,kuwadhalilisha wanasiasa, viongozi wa dini na wafanyi biashara kwa kuwabambika tuhuma nzito bila kuwa na ushahidi madhubiti, haihitaji kuwa na P.hD kuona kwamba vitu hivi vinamwumiza sana Kamanda Sirro ukitilia maanani mazingira ya seminari aliyokulia.

Kwa hiyo basi kwa mkutadha huu watu kama kamanda Sirro ndio watu wa kuombewa wamalize salama maana ni miongoni mwa watu wanaoishi kama digidigi ambae huwa hajui kama kesho ataiona,maana utekelezaji wa majukumu yake katika wakati uliopo haumpi matumaini kama siku itamalizika bila kutumbuliwa.
 
Back
Top Bottom