Kama wewe ni mwanamke wa Kiislam pitia hapa

Super Don

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,978
1,781
Utakuta mwanamke toka saa 6 anapika futari mpaka magharib adhana yamkuta jikoni nywele kitimutimu dira limejaa unga wa ngano umegandia na nyanya anamtengea mume chakula anuka kachori na katlesi,

Unapika futar nyingi mpaka ukilala hoi kama gogo halafu kuna wanawake Ramadan basi wajiachiaga wanakuwa rafu ukiuliza kafunga, shauri yenu hakuna kipindi wanaume wachepuka kama mwezi huu shuhudia fumanizi kibao anakuaga anaenda tarawehe anasali rakaa 8 nyingine ana malizia nyumba ndogo sikuambii 10 la mwisho ile kukesha msikitini

we we mtu anaishi Temeke eti taraweh anaenda kusalia kinondoni mtambani Temeke hakuna misikiti hizo pika pika zenu mnajisahau wanaume wenyewe wa Africa wanapata sababu kufunga sio sababu ukawe rafu pika futar kiasi upate muda wa kufanya ibada zako na kuhudumia ndoa yako,

pika kiasi wee siku moja futar 10 bado uji chai juice. pika mapema koga chana nywele zako kama mwehu, badilisha hilo dira lako lilogandia unga wa ngano, tia nyumba bokhoor hata mume karudi nyumba safi hainuki samaki na magimbi na wewe mwenyewe unamuandalia chakula msafi. shauri zenu usipoilela italala ifanyie lela isilale
 
Hivi unafikir wanawake wanaskia? Akili zao wanazijua wenyewe!
tapatalk_1494508699562.jpeg
 
Back
Top Bottom